JESHI LA POLISI LAWAONYA MAWAKALA WASIO FAA NAULI-ARUSHA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 13, 2022

JESHI LA POLISI LAWAONYA MAWAKALA WASIO FAA NAULI-ARUSHA

 

Abel Paul wa Jeshi la Polisi 
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia Kupitia kikosi cha usalama Barabarani Mkoani humo limewaonya baadhi ya mawakala wanaopandisha nauli kiholela kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kuwa halito wafumbia macho mawakala na wamiliki wa magari hayo.
 
Akiongea mapenda leo Decemba 13.2022 katika kituo kikuu cha mabasi yaendeayo mikoani Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO amesema kuwa Kwa sasa tiketi zinakatwa kwa mfumo wa kieletroniki ambapo amebainisha kuwa hato penda kusikia wamiliki na wakala wa mabasi hayo hawafuati utaratibu na maelekezo ya serikali kwa ukataji tiketi kwa mfumo wa kieletroniki.
 
Mwangamilo ameleza kuwa endapo atasikia mwananchi analalamika juu ya kupandishiwa nauli hatua kali zitachukuliwa kwa wakala atakaye bainika kukiuka maagizo ya serikali Pamoja na mliki kushindwa kusimamia watendaji wake.
 
Aidha SP Mwangamilo ameongeza kuwa madereva wanapaswa kufuata sheria za usalama Barabarani ili kuepusha ajali ambazo nimkuwa ziki ghalimu Maisha ya watu ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo halina ugomvi na madereva wanafuata sheria za usalama barabarani.
 
Nae Yahaya Mbwana ambaye Pia ni dereva wa basi linalofanya safari zake kati ya Singida na Arusha amewataka madereva wenzake kufuata sheria za usalama Barabarani ili kuepusha ajali ambazo chanzo chake ni ukikwaji wa sheria za usalama barabarani.
 

Nao baadhi ya mawakala wa mabasi yaendayo Mikoani wamesema changamoto kubwa kutoka kwa abiria wao ni uelewa mdogo juu ya mfumo mpya na bei elekezi ya serikali ambapo wamesema imekuwa chanzo cha malalamiko kwa abiria.
Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO akizungumza  mapenda leo Decemba 13.2022 katika kituo kikuu cha mabasi yaendeayo mikoani 
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad