BRAZIL YATOA ZAWADI KWA GWIJI WA SOKA PELÉ - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 6, 2022

BRAZIL YATOA ZAWADI KWA GWIJI WA SOKA PELÉ

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Wakati Gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, Pelé akiwa na hali mbaya, hospitalini akiendelea kupigania uhai wake, nchini Qatar timu hiyo imefuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 baada ya kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya taifa ya Korea Kusini, kwenye mchezo wa hatua ya 16 Bora ya Michuano hiyo uliochezwa kwenye uwanja wa ‘Stadium 974”, Ras Abu Aboud.
Brazil walipata ushindi huo kwa mabao ya Winga wake, Vinicius Jr kwenye dakika ya 7’, Mshambuliaji Neymar ambaye alifunga bao la pili kwa mkwaju wa Penalti dakika ya 13’, Richarlison alifunga bao la tatu dakika ya 29’ na Lucas Paqueta alipachika bao la nne dakika ya 36’. Bao la Korea Kusini lilifungwa na Paik Seung-ho katika dakika ya 75’.


Brazil watacheza hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo dhidi ya timu ya taifa ya Croatia baada ya wao kupata ushindi wa changamoto ya mikwaju ya Penalti 3-1 dhidi ya timu ya taifa ya Japan, kwenye mchezo uliopigwa katika uwanja wa Al Janoub.


Dakika 120’ zilitamatika timu hizo zikienda sare ya bao 1-1, mikwaju ya Penalti iliamua mshindi ambaye ni Croatia baada ya kupata mikwaju hiyo mitatu huku Japan wakipata mkwaju mmoja pekee.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad