Aleka Holdings yatoa msaada wa vifaa tiba hospitali ya Ocean Road - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 2, 2022

Aleka Holdings yatoa msaada wa vifaa tiba hospitali ya Ocean Road

  Kampuni ya utengenezaji na usambazaji ya vifaa tiba ya Aleka Holdings leo imetoa msaada wa barakoa za upasuaji kwa hospitali ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam.

Msaada huo wa barakoa hizo za upasuaji ni mwendelezo wa Kampuni  kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya afya kwa gharama nafuu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, mwakilishi wa Kampuni ya Aleka Holding alisema ‘Sisi Aleka Holding tunaunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata huduma kwa gharama nafuu. Tunafanya kazi ambayo inaguza moja kwa moja maisha ya Watanzania kila siku na san asana kwenye sekta ya afya. 

Wote tunaona jinsi serikali inapofanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya afya iliyo bora kwa gharama nafuu na kuja hapa kwetu leo kuja kutoa mchango wetu ni kuendeleza juhudi hizo’.

Aliongeza ‘Sisi ni Kampuni ya Kitanzania na vifaa vyetu vya tiba vinatengenezwa ndani ya nchi. Vifaa tiba vyetu vina ubora wa kimataifa na tunajivunia kuwa Kampuni ya kizalendo.

 Msaada huu ni muendelezo wa programu ya kurudisha kwa jamii na nataka kusema kuwa tutaendelea kufanya kazi pamoja na serikali kwenye kuwahudumia Watanzania wote’.

Akizungumza baada ya kupokea vifaa tiba hivyo, Mwakilishi wa hospitali ya Ocean Road Chausiku Chapuchapu aliwashukuru Kampuni ya Aleka Holding kwa kuguswa kwao na kuona umuhimu wa kuja kutuunga mkono.

‘Tumepokea msaada huu wa barakoa za upasuaji kwa moyo wa furaha na tunawashukuru sana wenzetu wa Aleka Holdings. Serikali yetu inafanya kazi kubwa kwenye huduma za afya lakini kwa sekta binafsi kuja kutuunga mkono ni kitu cha kushukuru sana. 

Tunawapongeza sana na tuna wakaribisha siku za mbele kwani bado mahitaji ya hospitali yetu hii ni makubwa’.
Mwakilishi wa Kampuni ya Aleka Holdings Steven Solar akimkabidhi sehemu ya barakoa 2,000 kwa Chausiku Chapuchapu ambaye ni Muuguzi Kiongozi Hospitali ya Ocean Road ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuhahakisha kuwa Watanzania tiba ya afya kwa gharama nafuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad