SAMSUNG A04E IMEZINDULIWA MSIMU WA SIKUKUU WATEJA KUPATA 75G BURE KWA MWAKA MZIMA KATIKA MADUKA YA AIRTEL - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 13, 2022

SAMSUNG A04E IMEZINDULIWA MSIMU WA SIKUKUU WATEJA KUPATA 75G BURE KWA MWAKA MZIMA KATIKA MADUKA YA AIRTEL

 

Dar es salaam 13 Dec 2023: Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kwa kutoa huduma bora kwa Smartphone imeungana na Kampuni ya vifaa vya elektroniki ya Sumsung kuzindua simu janja ya Samsung A04e itakayouzwa kwa gharama nafuu katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka itakayopatikana katika maduka ya Airtel na maduka ya Sumsung nchini

 

Meneja wa Mawasilianao na Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa Habari wakati wa kuzindua simu hiyo alisema Airtel kwa maranyingine tunaendelea kuunogesha msimu wa sikukuu kwa kuwapa fursa wateja kujipatia simu mpya na kujipatia zawadi za wapendwa wao na familia zikiwa na bando la BURE mwaka mzima. Lengo letu ni kuwafanya wateja wendelee kuunganishwa kigitali wakiwa popote na Airtel SUPA 4G.

 

Jitihadia nyingi tunazifanya ili kuendelea kupanua upatikana na matumizi yay a Smartphone kwa watanzania wote, Airtel kwakushirikiana na wadau wetu Samsung tunaahidi kuendelea kutimiza dhamira hii ya kupanua Maisha ya kidigitali kwa kuwaletea Simu Janja za Smartphone kwa gaharama nafuu ili kufikia asilimia 100 ya mipango ya kukuza Matumizi ya Internet.

 

Jackson aliongeza “Wateja wa Airtel watufurahia huduma bora za kidigitali kupitia mtandao wa Airtel supa 4G ulioenea nchi nzima. Ununuapo Samsung A04e tunatoa 75G BURE za data kwa mwaka mzima kwa wateja wote nchini.”

 

Akiongea katika uzinduzi huo wa ushirikiano, Mkuu wa Kitengo cha Simu za Mkononi wa Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga amesema, “Familia ya Samsung Galaxy A04e ipo hapa kwaajili ya kuwapa wateja wote nchini uzoefu mzuri wa kidijitali wa hali ya juu.”Utafurahia kuangalia maudhui uyapendayo kwenye scrini ya inch 6.5 yenye kamera ya megapixiel 13 na batrei inayokaa muda wa Zaidi masaa 24.Jipatie Galaxy A04e leo inayopatikana nchini kote katika maduka ya Airtel na Sumsung mikoa yote.

Simu hizi za Sumsung A04e  (32GB) kwa TZs 275,000 na hii ya GB 64 itapatikana kwa TZs

Meneja wa Mawasilianao wa Airtel Bw, Jackson Mmbando akiongea  na waandishi wa Habari wakati wa kuzindua simu  janja ya Samsung A04e inayouzwa msimu huu wa sikukuuu kwa gharama nafuu ikiwa na OFA ya bando la intaneti la Airtel GB 75 BURE kwa mwaka mzima. kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Simu za Mkononi wa Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga. Simu hii inakuwa na mdhamana wa miezi 24.Kushoto ni  Mkuu wa Kitengo wa Simu za Mkononi wa Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga akifafanua jambo wakati wa kuzindua Simu  janja Mpya ya Samsung A04e  itakayouzwa kwa ushirikiano na wadau wao Airtel katika msimu huu wa sukukuu  ikiwa na OFA ya bando la intaneti la Airtel GB 75 BURE kwa mwaka mzima. Pamoja nae kulia ni Meneja wa Mawasilianao wa Airtel Bw, Jackson Mmbando. Simu hii pia inakuwa na mdhamana wa miezi 24.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad