WAHITIMU CHUO KIKUU MZUMBE WATAKIWA KUWA WAZALENDO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 24, 2022

WAHITIMU CHUO KIKUU MZUMBE WATAKIWA KUWA WAZALENDO

 

 

NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO. 

 WAHITIMU  wa chuo kikuu Mzumbe wametakiwa kuwa wazalendo kwa kutunza na kusimamia  rasilimali za umma kwa maendeleo ya Taifa.

Wito huo umetolewa na  Mlau wa chuo kikuu Mzumbe Dk. Hawa Tundui alipokuwa akitoa nasaha kwa wahitimu wakati wa mahafali ya 21 ya chuo hicho.

Dk. Tundui alisema  kuwa uzalendo ni chachu na mtaji katika maendeleo ya nchi hivyo  kutumika na kutunza vizuri rasilimali kutasaidia Taifa kuondokana na hasara zinazoweza kutokea kutokana na kutokuwa na usimamizi bora.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu Mzumbe Dk. Saida Yahya Othuman alimshuku Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kushika nafasi hiyo.

Dk. Saida aliahidi kukisimamia chuo hicho ili kiweze kupiga hatua katika utekelezaji wa mipango yote ya chuo hicho.

Aliwataka wahitimu hao kwenda kuleta mageuzi kwenye jamii huku wakitambua kuwa mageuzi hayaji kwa kutumwa bali kwa kutumikia.

Naye kaimu makamu mkuu wa chuo kikuu Mzumbe Profesa William Mwegoha alisema kuwa jumla ya wahitimu 2631 watatunukiwa katika mahafali hayo.y















Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ally Mohammed Shein akimtunuku Shahada ya Uzamivu wahitimu wakati wa mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro yaliyofanyika leo Novemba 24,2022 mjini Morogoro.
   (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)






Meza kuu 






Sehemu ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe wakishangilia katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ally Mohammed Shein wakati wa mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro yaliyofanyika leo Novemba 24,2021 mjini Morogoro. 
(PICHZ ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)
Sehemu ya  Wazazi na wanafunzi.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad