UMATI UCHAGUZI WA CCM NI SALAMU ZA SUNAMI 2024-2025. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 20, 2022

UMATI UCHAGUZI WA CCM NI SALAMU ZA SUNAMI 2024-2025.

 

 

  Shaka asema idadi hiyo kubwa inatokana na uongozi bora wa Rais Samia

Asisitiza uchaguzi wa mwaka huu umevunja rekodi kwa kuwa haijawahi kutokea

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema mwitikio mkubwa wa wanachama kujitokeza katika uchaguzi kuanzia ngazi ya shina hadi taifa, ni salamu za kukubalika kwa Mwenyekiti wa Chama, Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia, amesema umati huo wa wanachama ni salamu za historia mpya katika kufanya vizuri katika uchaguzi wa 2024 na 2025 kwa kuwa viongozi watakaopatikana mwaka huu ndio wanaokwenda kukiongoza Chama katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. 

Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa Mkoa wa Magharibi katika ukumbi wa Banquet mjini Unguja.

“Viongozi hao wa Chama wa mikoa ndio watakaotoa mwelekeo wa ushindi wa CCM 2024 katika uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania Bara na 2025 uchaguzi mkuu kwa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema.

Shaka alisema kuwa CCM bado chaguo la umma kwa kuwa ni madhubuti, chenye muundo bora, mtandao mpana, viongozi imara, sera nzuri na kubeba matumaini na matarajio ya wananchi.

Alisisitiza kwamba mwitikio wa wanachama wa CCM kujitokeza kuomba uongozi umekuwa mkubwa kuliko wakati wowote katika historia ya Chama. 

Kwa mujibu wa Shaka, mwitikio huo ni kielelezo cha kukubalika, demokrasia pana na utendaji haki ndani ya Chama pamoja na imani kubwa waliyonayo wanachama kwa uongozi wa Mwenyekiti Rais Samia Suluhu Hassan. 

Aidha, alisisitiza kuelekea 2025 Chama kwa mujibu wa utaratibu na utamaduni wake hakina mpango wa kupata wagombea urais wengine kwa upande wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, badala yake kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kuendeleza umoja, mshikamano na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 ili itekelezwe kwa viwango kama ilivyoahidiwa kwa wananchi.

“Tabia na utamaduni huu wa kuahidi na kutekeleza umeendelea kuifanya CCM kutokuwa na mpinzani katika siasa za ushindani. Wanachama wa CCM fanyeni uchaguzi wa viongozi kwa sifa na uwezo wa kuongoza kwa maslahi ya Chama na nchi yetu,” alisema.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad