Shida ya maji kwa Wakazi wa Kata
ya Msamalo,Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kwa sasa itabaki kuwa historia
baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa maji utakaowanufaisha wakazi zaidi ya 4,000
pamoja na taasisi za kijamii kwenye eneo hilo.
Katika
kuhakikisha idadi kubwa ya watu inafikiwa na huduma ya maji safi na salama,
Shirika la Water Mission Tanzania kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wakala
wa Maji Vijijini (RUWASA) limezindua mradi huo ambao utapunguza adha ya kufuata
maji umbali mrefu kwa wakazi 4,085 wa eneo hilo.
Pia,
mradi huo utazinufaisha zaidi ya kaya 730 pamoja na taasisi mbalimbali za
kijamii ikiwamo kliniki, masoko pamoja na taasisi za kidini jambo ambalo
linaashiria ustawi wa watu pamoja na shughuli za kijamii na kiuchumi.
Akizungumza
wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Water Mission Tanzania, Benjamin
Filskov alisema utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya mkakati wa shirika hilo
katika kuunga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata
maji safi na salama karibu na makazi yao.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Water Mission
Tanzania, Benjamin Filskov alieleza kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha
wananchi wanakuwa na mfumo thabiti wa kupata maji safi na salama karibu na
makazi yao.
“Tunatambua uwepo wa mahitaji makubwa ya maji
kwenye eneo hili na leo hii tunayo furaha kuzindua mradi huu ambao utasaidia
kupunguza adha ya maji kwa wakazi wa eneo hili.Mafanikio hay ani ishara ya
ushirikiano wet una Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) na Wizara ya Maji katika
kusaidia jitihada za Serikali kufikisha huduma za maji kwa watu wote,” alisema.
Akizindua
mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandishi Antony Sanga alisema
kukamilika kwa mradi huo ni utekelezaji wa ahadi za Serikali katika kupunguza
kero ya maji kwa wananchi na kwamba utasaidia kuboresha maisha ya wakazi wa
eneo hilo.
“Tunamshukuru
sana Rais wetu, wakati wa kampeni aliahidi kwamba tutawapelekea wananchi wetu
huduma ya maji hivyo huu ni upendo wake kwenu wana Msamalo,” alisema.
Aliwataka
wakazi wa Msamalo kushirikiana ili kuendeleza mradi huo ili uwe endelevu kwa
manufaa kwa vizazi vijavyo.
Mradi
huo unatumia nishati ya jua ‘Solar’ ambapo maji yanavutwa kutoka kwenye kisima
na kwenda kwenye kituo cha kusafisha na kutibu maji na baadaye yanapelekwa kwenye
vituo 18 vilivyopo karibu na makazi ya watu.
1.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maji, Mhandishi Antony Sanga pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Water Mission Tanzania, Benjamin Filskov wakikata utepe kuashiria uzinduzi
ramsi wa mradi wa maji wa Msamalo wilayani Chamwino-Dodoma.Mradi huo utatoa
huduma ya maji safi na salama kwa wakazi zaidi 4,000 pamoja na taasisi za
kijamii.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Antony Sanga pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Water Mission Tanzania, Benjamin Filskov wakinywa maji safi na salama kutoka kwenye mradi wa maji wa Msamalo uliozinduliwa jana.Mradi huo utasaidia kutoa mani safi na salama kwa wanakijiji zaidi ya 4,000 waishio kwenye eneo hilo.
1. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandishi Antony Sanga akimtwika ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Msamalo Wilayani. Chamwino mkoani Dodoma baada ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Msamalo ambao utahudumia kaya zaidi ya 730 pamoja na taasisi za kijamii zikiwamo shule, kliniki pamoja na taasisi za dini.
No comments:
Post a comment