HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 2, 2019

WAZIRI MKUU AFUNGUA WIKI YA SHERIA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza matembezi ya kuadhimisha Wiki ya Sheria, jijjini Dodoma  Februari 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifanya mazoezi ya viungo nje ya viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019, baada matembezi ya kuadhimisha Wiki ya Sheria, kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia mifumo ya kisasa ya Mahakama Mtandao wakati alipokagua mabanda katika kuadhimisha Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019 kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tehama Kalege Anock, Athumani Kanyegezi na Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa picha na Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba hadija Mwema, wakati alipotembelea banda la Mkemia Mkuu wa Serikali katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Fatma Karume, wakati alipotembelea mabanda katika Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu na Mtendaji Mkuu RITA, wakati alipotembelea banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini RITA, katika Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019, kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma na Afisa Usajili Msaidizi RITA Joseph Mwakatobe. 
 Wananchi waliyohudhuria katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma, akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi waliyohudhuria katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019.

*Asema Serikali ni mdau muhimu wa Mahakama
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeendelea kushirikiana na Mhimili wa Mahakama katika kuhakikisha huduma bora za utoaji haki zinawafikia wananchi kwenye maeneo wanayoishi kwa wakati.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ni mdau muhimu wa Mahakama na inafuatilia kwa karibu changamoto zote zinazoikabili pamoja na wadau wengine katika mfumo wa utoaji haki.” 

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Februari 2, 2019) wakati akifungua wiki ya Sheria Tanzaniakatika viwanja wa Nyerere Square jijini Dodoma. Ametoa wito kwa wananchi watembelee mabanda ya maoneshohayo.

Amesema kupitia wiki ya sheria wanachi watapata elimu kuhusu masuala ya sheria pamoja na kushuhudia na kunufaika na maboresho yanayofanywa na Mahakama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika utoaji haki.

Waziri Mkuu amesema jambo hilo ni jema kwani masuala ya kisheria si mepesi kujulikana kwa kila mwananchi na kwa sababu hiyo, wananchi wengi wamekuwa na uelewa mdogo wa masuala hayo ya kisheria. 

Amesema wananchi wengi hawajui taratibu na mienendo ya kimahakama na wakati mwingine wanakosa au kupoteza haki zao kwa kigezo cha kutofuata taratibu ili kupata haki zao hizo.

“Nitoe rai kwa wananchi watumiae ipasavyo fursa hii ya Wiki ya Sheria inayoambatana na maonesho kwa lengo la kupata elimu na huduma mbalimbali hususan za kisheria.”

Akizungumzia kuhusu dhamira ya Mahakama kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuleta mabadiliko kwenye utoaji haki, amesema ni hatua nzuri na itasaidia kuboresha utoaji wa haki kwa wakati.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewasihi katika matumizi hayo ya mifumo ya TEHAMA wasikatishwe tamaa na changamoto zitakazojitokeza kwani mara nyingi kitu kipya chochote hakikosi changamoto za hapa na pale. 

“Binafsi naunga mkono uamuzi wa dhati wa Mhimili wa Mahakama kutumia TEHAMA katika usajili wa mashauri. Uamuzi huo unakwenda sanjari na azma ya Serikali ya kuhakikisha TEHAMA inatumika vema kwenye taasisi za umma kwa lengo la kutoa huduma bora na kwa wakati.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema matumizi bora ya TEHAMA yataipunguzia Serikali na mihimili mingine ya dola gharama za uendeshaji hususan katika utoaji huduma kwa wnanchi.

Amesema lengo la Serikali ni kuona kuwa huduma bora zinawafikia wananchi kwa urahisi na vilevile, zinapatikana wakati wote. “Nitoe wito kwa wadau muhimu wakiwemo Mawakili wa Serikali na Mawakili wa Kujitegemea, nao kutumia mifumo ya TEHAMA katika kusajili mashauri na wala wasiwe wao wa kwanza katika kulaumu na kubeza.” 

Amesema Mawakili wote wa Serikali na Kujitegemea, wanapaswa kuwa sehemu ya kutatua changamoto zitakazoibuka katika matumizi ya mifumo hiyo ya TEHAMA kwa kuwasilisha mapendekezo kuhusu namna bora ya kuiboresha. 

Ameongeza matumizi ya TEHAMA siyo tu yatawawezesha kutoa huduma kwa wakati, lakini yataweka uwazi ambao utawapunguzia malalamiko mengi kuhusu watumishi wenu na utoaji haki. 

Waziri Mkuu amewataka watumie vema Wiki ya Sheria kwa ajili ya kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu mapinduzi ya matumizi ya TEHAMA yanayoendelea Mahakamani.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma amesema kwa kipindi cha wiki nzima, maonesho ya Wiki ya Sheria yatafanyika jijini Dodoma pamoja na kwenye Mahaka zote nchini, kuanzia ngazi ya wilaya.

Pia, Jaji Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa vijiji, kata, wilaya, mkoa, idara na wizara, wabunge, majaji, mahakimu na watumishi wa umma wahudhurie maonesho hayo ya Wiki ya Sheria.

Ametolea mfano banda la maonyesho la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu litawakumbusha kuwa mamlaka yao mihimili mitatu ya dola yanatokana na nguvu ya sheria, nguvu ambayo haimuonei mwananchi yeyote.

Jaji Mkuu amesema watu watakaoshiriki katika maonesho hayo kwa kutembelea mabanda watumie nafasi hiyo kujifunza na kutathmini umuhimu na hadhi ya mfumo wa kimahakama katika kustawisha maisha yao pamoja na kuwasaidia kupata haki kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya kufungua maadhimisho hayo ambayo kwa mara ya kwanza yamefanyika nje ya jiji la Dar es Salaam, Waziri Mkuu alishiriki matembezi ya kilomita tano pamoja na Jaji Mkuu na viongozi wengine yaliyoanzia Mahakama Kuu Dodoma hadi viwanja vya Nyerere Square na kisha alitembelea mabanda.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad