HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 3 February 2019

MITAA MITATU KATA YA PANGANI WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA VIKAWE


NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

KERO kubwa ya maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili kipindi kirefu ,wakazi wa mitaa mitatu ya miwale, vikawe shule na vikawe Bondeni, kata ya Pangani ,Kibaha, mkoani Pwani imepata mkombozi baada ya kukamilika kwa mradi wa maji ambao utapunguza kero hiyo. 

Wakizungumza wakati mbunge wa jimbo la Kibaha Mji, Silvestey Koka alipokwenda kukagua miradi ya maendeleo kata ya Pangani, walieleza kipindi cha nyuma walikuwa wakitumia maji ya visimani yasiyo salama kiafya. 
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amkitwisha ndoo ya maji mmoja wa akina  mama


Grace Sinzuki na Maua Mussa walisema walitumia muda mwingi nyakati za usiku na mchana kwa ajili ya kutafuta huduma hiyo. "Visima vilikuwa mbali kufikika ,tulikuwa tunaacha kulala waume zetu kitandani kwenda kusaka maji hivyo mradi huu utakuwa ni mkombozi mkubwa "alifafanua Grace. 

Maua alisema, hivi karibuni Koka alifanya ziara Vikawe na kupata malalamiko juu ya kusuasua kwa mradi huo ,na alilazimika kuunda kamati ndogo ili kufuatilia DAWASA Bagamoyo ambayo sasa imeuchukua mradi na kuanza kazi. 

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka aliahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tano na mamlaka zinazohusika kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika baadhi ya maeneo. 

Koka alieleza lengo la serikali ni kumtua ndoo mama kichwani, hivyo ni wajibu wake kusimamia kero iliyopo ili wananchi wasambaziwe maji majumbani. Nae mhandisi wa miradi ya DAWASA wilayani Bagamoyo ,Hamad Omary alisema kwamba lengo lao ni kuhakikisha wanaboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi .

Alifafanua juhudi zinaendelea kufanyika ili wananchi waweze kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu ikiwa ni pamoja na kufufua vizimba ambavyo vilikuwa vimekufa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad