HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 28, 2019

Misri kuwanoa Ocean Road katika saratani ya matiti

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) kupata watalaam Bingwa  wa Misri katika kuwaongezea ujuzi katika kansa ya matiti. Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu  wa Taasisi hiyo Dkt.Julius Mwaiselage amesema kuwa mafunzo yatafanyika kwa wiki moja kwa madaktari na wauguzi 120.

Mwaiselage amesema amesema kuwa Misri wana uwezo mkubwa katika katika saratani ya matiti hivyo watatupa uwezo katika utoaji wa huduma za saratani hiyo. Aidha katika ujio huo madaktari Bingwa hao katika taasisi ni kuanzisha huduma ya upasuaji hali ambayo itaongeza uhudumiaji wa wagonjwa wa saratani ya matiti. Aidha amesema  kuwa watalaam hao wataboresha  ukusanyaji wa takwimu za watu wenye saratani kutokana jinsi walivyoanzisha nchini humo.

Dkt.Mwaiselage amesema kuwa saratani saratani ya matiti iko katika kiwango kikubwa ikilinganishwa na ile ya mlango wa kizazi na Misri na wako katika kiwango cha juu lakini wameweza kukabiliana. Nae Mkuu wa Kitengo cha Wizara ya Afya wa Nchini Misri Dkt.Nadia Badawy amesema wamekuja Tanzania katika katika kutoa elimu ya afya katika eneo la saratani.
Amesema katika ziara hiyo watatoa elimu kwa njia mbalimbali kuhusiana na saratani ya matiti.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt.Julius Mwaiselage akiwapa maelezo madaktari Bingwa wa Misri wakati akiwa waonesha sehemu mbalimbali za Taasisi hiyo.
 Mkuu wa Kitengo Habari wa Wizara ya Afya nchini Misri Nadia Badawy akizungumza namna walivyojipanga katika kuwanoa wataalam katika Taasisi ya Ocean Road.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya  Ocean Road Dkt.Julius Mwaiselage akizungumza na waandishi wa habari wakati madaktari Bingwa wa Saratani kutoka Misri waliokuja kutoa mafunzo kwa madaktari na wauguzi wa Taasisi hiyo
Mratibu wa Saratani ya Uzazi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Safina Yuma akizungumza kuhusiana na ujio na madaktari Bingwa kutoka Misri.
 Picha ya namna wanavyopima saratani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad