HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 18, 2018

WATANZANIA WATEULIWA NA CAF KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA MECHI ZA KUFUZU AFCON



Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi kutoka nchini Tanzania kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 Cameroon kati ya Seychelles na South Africa 
utakaochezwa Uwanja wa Stade Linite Oktoba 16,2018.


Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Mfaume Ali Nassoro akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Ferdinand Chacha, Mwamuzi msaidizi namba 2 Alli Kinduru na Mwamuzi wa akiba Elly Sasii. Mtathmini waamuzi anatokea Uganda Ronnie Kalema na Kamishna wa mchezo anatokea France Yves, Jean-Baptiste Etheve. 


Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) limemteua Bwana Ahmed Idd Mgoyi kuwa kamishna wa mchezo wa Kufuzu kucheza AFCON 2019 Cameroon, mchezo ambao utazikutanisha Malawi na Cameroon mchezo utakaochezwa Oktoba 16, 2018 
Kamuzu Stadium katika Mji wa Blantyre


Naye Leslie Liunda ameteuliwa kuwa mtathmini Waamuzi mchezo utakaowakutanisha Congo DR na Zimbabwe utakaochezwa Kinshasa Complexe OmniSports Stade Des Martyrs Oktoba 13,2018.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad