HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 12, 2018

TAWA yawakamata,pokonya baiskeli 60, Nyaya 100 za majangiri

  Ofisa Kampuni ya uwindaji wa Kitalii ya Mkwawa Hunting Safari Benson Kibonde akisisitiza jambo mbele ya Afisa Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA),Twaha Twaibu kushoto na Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Magharibi-Msolwa Pori la Akiba Selous Augustine Ngimilanga.
 Afisa Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA),Twaha Twaibu kushoto akiwa na Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Magharibi-Msolwa Pori la Akiba Selous Augustine Ngimilanga wakiangalia baiskeli zilizotumiwa na majangiri kubebea wanyamapori.
 Mofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), katika Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi -Msolwa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Kijiji cha Msolwa Station Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kutembelea Shule ya Msingi Ukombozi kujionea mchango wa uhifadhi kutoka kampuni za uwindaji wa kitalii. 
 Mofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), katika Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi -Msolwa wakiwa katika picha ya  na viongozi na Kijiji cha Msolwa Station Kilombero mkoani Morogoro baada ya kutembelea jengo la Ofisi ya Kijiji cha Msolwa Station linalojengwa kwa fedha kutoka kampuni za uwindaji wa kitalii. 
Afisa habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Twaha Twahibu akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa Kijiji cha Msolwa Station kinachopakana na Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi-Msolwa mkoani Morogoro.

NA RIPOTA WETU,KILOMBERO
MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), katika kipindi cha mwaka 2017/18 imekamata baiskeli 60 za watuhumiwa wa ujangiri zikiwamo Nyaya zaidi ya 100 ndani ya Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi- Msolwa.

Mkuu wa Kanda hiyo, Augustine Ngimilanga alisema pamoja na kukamata nyenzo hizo askari wa doria pia walikamata watuhumiwa wa ujangiri waliofunguliwa kesi 92 zinazoendelea Mahakama ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

“Watuhumiwa 18 wameshasomewa kesi zao na kuhukumiwa baadhi wamefungwa miaka mitatu na wengine miaka tisa jela,” alisema Ngimilanga na kuongeza:

“Tumeweka mkakati wa kuhakikisha maeneo yote yanakuwa na ulinzi wa doria muda wote, hii ni pamoja na kukabiliana nao kabla hawajaingia na kufanya uharibifu,” alisema.

Ngimilanga alizitaja changamoto katika kukabiliana na ujangiri zinachangiwa na hali ya umasikini ya wananchi katika vijiji vinavyopakana na pori hilo.

“Baadhi ya wananchi wameona njia pekee ya kujipatia kipato ni kufanya ujangiri wa kuwinda wanyama na kuvua samaki kwenye mito ndani ya Pori la Akiba.

“Mbali ya kukamata tunaowakuta, tumeendelea pia kutoa elimu maeneo mbalimbali ya vijiji ikiwamo mikutano ya vijiji kwa kuwaelimisha na kuwapa mifano ya umuhimu wa kutunza haya maeneo,”alisema.

Alisema ili kuwasaidia kutoshiriki vitendo vya kijangiri wamekuwa wakiwapa elimu ya ujasiriamali wa ufugaji nyuki kwa ajili ya kuvuna asali na kuuza kwa lengo la kujiongezea kipato.


“Tumewasaidia kupata ufadhili wa mizinga kutoka kwa wawekezaji ili waendeshe shughuli za ufugaji kwenye msitu wa Magombela,” alisema Ngimilanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad