HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 14, 2018

SIKU YA MOYO DUNIANI KUADHIMISHWA SEOTEMBA 29 KWA KUPIMA MAGONJWA YA MOYO

Mwenyekiti wa chama cha madaktari wa moyo nchini Dkt. Robert Mvungi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati alipotambulisha siku ya moyo duniani ambayo itafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Septemba 29,2018.

Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
MAADHIMISHO ya siku ya moyo duniani yenye kauli mbiu ya "My "Heart, Your hear" (Moyo wangu, moyo wako) yanatarijiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu katika Mikoa mbalimbali na jumbe mbalimbali  kuhusu ugonjwa wa moyo kutolewa.

Akizungumza na vyombo vya habari Mwenyekiti wa chama cha madaktari wa moyo nchini Dkt. Robert Mvungi ameeleza kuwa sherehe hizo katika Mkoa wa Dar es salaam zitaongozwa na kiongozi kutoka Wizara ya Afya na zitafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja na klabu mbalimbali za mazoezi kutoka Wilaya zote zitakutana viwanjani hapo wakitokea katika maeneo yao.

Aidha ameeleza kuwa hospitali mbalimbali zitashiriki katika maadhimisho hayo zikiwemo zile za hospitali za serikali na watu binafsi kama vile Mloganzila, Amana, Temeke, Aga Khan na Kairuki hospitali.

Pia amesema kuwa Mikoa mbalimbali itaadhimisha siku hiyo katika maeneo yao ikiwemo Moshi katika viwanja vya hospitali ya Kilimanjaro Christian Centre,  Mwanza wataadhimisha siku hii katika viwanja vya hospitali ya Bugando, na Mbeya wataadhimisha siku hiyo  katika viwanja vya hospitali ya rufaa ya Mkoa na maandamano katika Mikoa hiyo itaanzia kwenye ofisi za wakuu wa Mikoa na kumalizika kwenye maeneo yaliyopangwa ambapo upimaji wa magonjwa ya moyo na elimu itatolewa na kwa Mkoa wa Dodoma maadhimisho hayo yatafanyika katika hospitali ya Benjamini Mkapa.

Mvungi amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili waweze kujua namna ya kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo yanaweza kuzuilika kwa asilimia 80 kwa kuishi maisha ya afya nzuri, kufanya mazoezi, kutovuta sigara na kuepuka mwili mkubwa(obesity.)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad