HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 21 September 2018

NEC YAKANUSHA TUHUMA ZA CHADEMA


Na Bartholomew Wandi


Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia amekanusha Tuhuma mbalimbali zilizotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) zinazohusu Uchaguzi Mdogo wa Ubunge wa Majimbo mawili ya Monduli katika Halmashauri ya Wilaya Mnduli, jijini Arusha na Ukonga katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam pamoja na Kata Ishirini na Tatu (23) Tanzania Bara.


Dkt. Kihamia wakati anaongea na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi alikanusha kwamba Tume haijaongeza vituo kumi na sita (16) hewa vya kupigia kura katika Jimbo la Ukonga kama CHADEMA wanavyodai bali bali Tume imetumia Daftari lile lile la Wapiga kura na vituo vile vile vya kupigia kura la mwaka 2015.

“Vitu vya kupigia kura vilivyotumika mwaka 2015 katika Jimbo la Ukonga ni 673 na havikupungua hata kimoja au kuongezeka hata kimoja”. Alisema Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Mkurugenzi alisema kuwa wananchi wasipotoshwe na wanasiasa na hao CHADEMA wafuate utaratibu wa kisheria badala ya kukumbilia kwenye vyombo vya habari na kama kweli wanaamini vituo hiyo hewa vipo Mahakama itatengua matokeo.

Dkt. Kihamia pia alikanusha madai ya CHADEMA kuwa mawakala wake wote walifukuzwa walifukuzwa Vituoni. Mawakala waliofukuzwa vituoni ni wa vituo vinne tu.

Mkurugenzi alibainisha sababu ya kufukuzwa kwa mawakala hao wa vituoni kwa kuwa walienda kwenye vituo ambavyo sivyo walivyopangiwa na mwingine alifukuzwa kwa kuwa alienda kituoni bila kuapishwa baada ya kuchaguliwa na chama chake siku hiyo hiyo ya Uchaguzi baada ya waliochaguliwa mwanzoni na kula kiapo kutofika vituoni.

Mkurugenzi aliongeza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwatuma Makamishna na Maofisa wake kwenye maeneo yote ambayo yanafanya uchaguzi ili kufuatilia malalamiko ya vyama vya siasa kama yana ukweli wowote. Kwa Mfano Katika kituo cha Darajani CHADEMA walilalamika kuwa Wakala wake hakuwepo kituoni, lakini baada ya Mkurugenzi Tume kuomba namba ya Wakala huyo na kumpigia Simu mwenyewe alijibu kuwa yupo kituoni .

Mkurugenzi wa Uchaguzi alifafanua pia, kuwa Tume bado haijachelewa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa sababu muda bado upo mpaka ufike Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020. Wakati wowote Daftari litaboreshwa na waliotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea wataandikishwa.

Hata hivyo, Mkurugenzi alielezea kuwa baada ya Uchaguzi Mdogo kufanyika, huwa Tume inafanya tathmini ya uchaguzi huo na kama kuna changamoto huwa zinafanyiwa kazi kazi kuzirekebisha au kuziondoa ilizisijitkeze katika Chaguzi Ndogo nyingine zinazofuata.Kuhusu tatizo la Wapiga kura kujitokeza wachache kwenye Chaguzi Ndogo, Mkurugenzi aliwaomba waandishi wa habari wafanye utafiti, kwani duniani kote chaguzi hizo ndogo huwa na wapiga kura wachache sana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad