HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 12, 2018

DC KAWAWA APIGA MARUFUKU WANAOSHIRI KUKARIBISHA MIFUGO KIHOLELA

 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa akizungumza na watendaji na madiwani. 
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya watendaji na madiwani wa Bagamoyo wakifuatilia yaliyojiri kwenye kikao cha baraza.

NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 
MKUU wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa ametoa onyo kwa baadhi ya viongozi wa vijiji na watendaji wanaoshiriki kukaribisha wafugaji bila utaratibu na waache mara moja ,kwani ndio kichocheo cha uvunjifu wa amani na migogoro baina yao na wakulima.

Aidha, amepiga marufuku wafugaji kuingiza mifugo yao kiholela wilayani humo pamoja na maeneo ya wawekezaji ili kuondoa migogoro inayojitokeza mara kwa mara.

Rai hiyo aliitoa ,wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na madiwani na watendaji wa halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo. 

Zainab alieleza ,wapo viongozi wanaokula na wafugaji suala linalosababisha ongezeko la mifugo kwenye maeneo yasiyo rasmi. 

Alisema kuwa, kumekuwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji kutokana na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima ama wawekezaji hali inayosababisha mapigano.

“Nasema inatosha, wilaya kwasasa ina mifugo hiyo 300,000 yaani halmashauri ya Chalinze ina ng'ombe 240,000 na Bagamoyo ng'ombe 60, 000,"

Zainab alielezea, baaadhi ya viongozi wamekuwa wakijihusisha na uingizaji mifugo kwa kutumia njia ambazo ni kinyume cha sheria hali ambayo inasababisha madhara makubwa ndani ya jamii .

Hata hivyo alisema, NARCO inaanzisha maeneo ya wafugaji na inatenga heka 100,010 ambapo watakodishwa ndani ya miezi mitatu ng'ombe mmoja sh. 10,000 na ukiisha muda huo unaanza mkataba upya. 

Zainab alifafanua, njia hiyo itapunguza ongezeko la mifugo hiyo, hivyo madiwani na watendaji wampe ushirikiano kuwasiliana na wafugaji kuwashirikisha kwenye mpango huo. 

Mkuu huyo wa wilaya ya Bagamoyo, aliahidi kukutana na wafugaji kuzungumza nao kuhusu kuheshimu mipaka isiyowahusu na juu ya kupeleka mifugo yao NARCO.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Latu alisema wamepokea maelekezo hayo kwani anaamini ni semina elekezi kwa wataalamu ,madiwani, watendaji na wananchi ili kuhakikisha wanaleta maendeleo .

Nae diwani wa kata ya Yombo, Mohammed Usinga alisema changamoto ya kuingizwa makundi ya mifugo ni kero kubwa .

Aliwataka wakulima na wafugaji waheshimiane ili kuishi kwa amani. 


Usinga aliahidi kwa niaba ya madiwani wengine kumpa ushirikiano mkuu huyo wa wilaya ili kudhibiti kero hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad