HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 29 August 2018

MSAJILI NGOs AWAHIMIZA WADAU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUTILIA MKAZO UTEKELEZAJI WA SERA ZA MAENDELEO

Na WAMJW Dodoma
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba ameyataka wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutilia mkazo katika kutekeleza Sera za Maendeleo zilizopo katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) ili kufanikisha juhudi za Serikali katika kuletea wananchi Maendeleo.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma.

Bw. Katemba amesisitiza kuwa Mashirika hayo yanapaswa kuwasilisha mipango yao kwa Msajili ili kuweza kuwa na Mpango mkakati mmoja wa kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.

Ameongeza kuwa suala la Maendeleo ni mtambuka na linapaswa kutekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali, Wadau na wananchi ili kufanya shughuli za Maendeleo kuwa endelevu.

Kwa upande wao wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakiwakilishwa na Mwakilishi wa Shirika la Care International Bi. Zenais Matemu amesema kuwa wadau ni wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni muhimu katika Maendeleo hivyo kuiomba Serikali kuendelea kushirikiana ili kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii imepanga kukutana na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mara moja kila baada ya miezi mitatu kujadiliana masuala mbalimbali ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo nchini.


 Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Jijini Dodoma katika kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.
Watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Idara Kuu Maendeleo ya Jamii pamoja na wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilishwa kuhusu ushirikiano kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Serikali katika kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad