HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 29, 2018

MATUMIZI YA POMBE YANA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII

MTANDAO wa Kudhibiti Madhara ya Matumizi ya Pombe (TAAnet) umeeleza kuwa matumizi makubwa ya pombe ni chanzo kikubwa cha matatizo hasa ugomvi na mifarakano katika familia.

Aidha mtandao huo umesema asilimia nne ya vifo vitokeavyo duniani na asilimia nne ya magonjwa yasitoambukizwa usababishwa na matumizi makubwa ya pombe yanayofanika kwa sasa.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam Jana na Mjumbe wa bodi katika mtandao huo, Dk. Mashombo Mkamba wakati wa semina ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu madhara ya matumizi ya pombe.

Alisema licha ya pombe kusababisha matatizo hayo pia inaelezwa kuwa ni moja ya visababishi vikubwa vya aina mbalimbali ya saratani zinazotesa baadhi ya watu nchini na duniani kwa ujumla.

"Najua ni vigumu kwa baadhi ya watu wanaotumia pombe kuacha Ila upo uwezekano wa kuiacha kama utaamua kwani hakuna faida yoyote inayotokana na unywaji wa pombe," alisema na kuongeza kuwa.

"Licha ya pombe kuwa chanzo kikubwa cha mapato ya serikali duniani kote,lakini usababisha ajali nyingi zinazosababisha vilema  na kupoteza maisha ya watu wengi," alisema.

Aidha alisema inakadiliwa katika kila mwaka lita 2.4 bilioni za pombe za kienyeji utengenezwa na kunywewa hapa nchini na kusema hiyo ni idadi kubwa ya pombe inayonywewa na watu.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa TAAnet Sophia Komba alisema yapo magonjwa zaidi ya 120 usababishwa na matumizi ya pombe hivyo ameitaka jamii kubadilika kuacha matumizi ya vilevi kwani havina maendeleo wala faida yoyote.
Waandishi wa habari wakiwa katika semina ya siku moja inayohusu madhara ya matumizi ya pombe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad