HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 31, 2018

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHABAINI KUONGEZEKA KWA KASI UKATILI WA KINGONO,UBAKAJI KWA WATOTO

Na Leandra Gabriel, Glogu ya jamii
KITUO cha Sheria na haki za binadamu (LHRC)  kimezindua ripoti ya nusu mwaka ikionesha hali ya haki za binadamu katika kipindi cha miezi 6 ya mwaka 2018 yaani kuanzia Januari hadi Juni.

Akizungumza na wanahabari katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho na Wakili  Anna Henga ameeleza kuwa ripoti hiyo imeandaliwa kwa kutumia vyanzo mbalimbali kama vile jeshi la polisi, ripoti za mashirika mbalimbali pamoja na vyombo vya habari na ripoti hiyo imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni haki za kiraia na kisiasa, haki za kijamii na haki za za makundi maalumu.

Henga ameeleza kuwa ripoti hiyo imeibua mambo muhimu ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa ukatili dhidi ya watoto hasa ukatili wa kingono na ubakaji mara tatu zaidi ukilinganisha na kipindi cha mwaka 2017 na hii ni kwa kulinganisha matukio 12 kwa mwaka 2017 kufikia matukio 533 kwa mwaka 2018 na kati ya matukio 6376 ya ukiukwaji wa haki za watoto  matukio 2365 yametokana na ubakaji na matukio 533 ni ulawiti 

Pia ameeleza kuwa ukatili dhidi ya wanawake umeongezeka  hasa wa kingono na mwili ambapo matukio ya ubakaji yaliyoripotiwa  kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu yamefika1218 ikikadiriwa idadi ya wanawake 203 hubakwa kwa mwezi.

Aidha ameeleza kuwa matukio ya mauaji wa kutokana na imani za kishirikina yamepungua kutoka matukio 172 hadi 106, na ajali za barabarani zinazosababisha vifo zimepungua huku hofu kubwa ikiongezeka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi 2019/2020.

Pia amesema kuwa haki ya kujieleza imeendelea kuminywa na hii ni baada ya kutungwa kwa kanuni za maudhui mtandaoni na changamoto katika mazingira ya elimu hasa upungufu wa matundu ya vyoo mashuleni akitolea mfano wa shule ya Msingi Ichenjezya mkoani Songwe yenye wanafunzi wapatao 1300 wanaotumia matundu 8 pekee.

Kwa upande Mtafiti anayefanya kazi na kituo hicho bw. Fundikira Wazambi ameeleza kuwa matukio ya ukatili kwa watoto yameongezeka kutoka 4,728 kwa mwaka 2017 hadi kufikia matukio 6,376 mwaka huu na matukio hayo ni pamoja na ubakaji na ulawiti na suala la ndoa za utotoni na ukeketaji bado ni changamoto.

Kwa upande wa wanawake matukio ya ukatili  dhidi ya wanawake yameongezeka hasa kimwili na kingono takimwu zinaonesha kwa nusu mwaka pekee wanawake 203 wamebakwa pia rushwa ya ngono makazini na vyuoni bado ni changamoto kubwa na hii ikihusisha wanahabari wa kike.

Kuhusiana na haki za kiraia na kisiasa yaliyoelezwa na mtafiti huo ni pamoja na mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola, kuminywa kwa uhuru wa kujieleza huku haki ya kuishi ikiimarika kidogo kwa kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu.

Haki za kijamii zimeelezwa kuwa sera ya elimu bure imewezesha watoto wengi zaidi kupata elimu ukilinganisha na miaka ya nyuma licha ya kuwepo na changamoto ikiwemo upungufu wa matundu ya vyoo mashuleni.

Pia imeelezwa kuwa kuna upungufu wa wafanyakazi wa sekta ya afya baada ya zoezi la wenye vyeti feki kupita, pia watu wenye ulemavu wameendelea kukumbwa na changamoto za unyanyapaa kwenye nyanja za elimu, ajira na miundombinu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad