HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 31, 2018

KILELE CHA MAFANIKIO KWA MWANAMICHEZO NI KUIWAKILISHA NCHI KIMATAIFA: WAZIRI MWAKYEMBE

 Katibu Mkuu  Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi   akizungumza leo Jijini Dodoma na wachezaji walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  (hawapo katika picha) ambapo timu ya mpira wa miguu wanawake waliibuka washindi wa kwanza, katikati ni Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Harrison Mwakyembe na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe  akisisitiza jambo kwa wachezaji walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Masharik (hawapo katika picha), wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji hao leo Jijini dodoma, kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Zanzibar Bw.Hamis Alli Mzee,anayefuata ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Susan Mlawi na  kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe  akifurahi pamoja na viongozi wengine wa Wizara  leo Jijini Dodoma baada ya  kupokea kombe kutoka kwa Nahodha wa timu ya mpira wa miguu wanawake Bi. Asha Rashidi (hayupo katika picha).
 Baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars wakimsikilza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) wakati wa halfa ya kuipongeza timu hiyo leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa timu  zilizoshiriki  mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo timu ya mpira wa miguu wanawake waliibuka washindi wa kwanza.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja  na wachezaji wa timu ya Karate.

Katibu Mkuu  Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi (katikati)  akifurahi pamoja na wachezaji wa mpira wa pete  leo Jijini Dodoma  baada ya timu hiyo kurejea ikitokea Bujumbura nchini Burundi ilipokuwa ikishiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo iliibuka mshindi wa pili.
(Picha na Shamimu Nyaki-WHUSM)


Na Shamimu Nyaki –WHUSM
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa mwanamichezo anayepaswa kujivunia mafanikio katika michezo ni yule ambaye ameiletea nchi sifa nzuri ya ushindi.

Hayo ameyasema leo Jijini Dodoma katika halfa ya kuzipongeza timu zilizoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika mjini Bujumbura nchini Burundi ambapo timu ya mpira wa miguu ya wanawake waliibuka washindi wa kwanza.
 “Sasa naona wachezaji  wetu mmebadili muelekeo kwa kuweka juhudi na kuhakikisha mnailetea heshima nchi yetu kwa kuja na kombe la ushindi, hiki ndio kilele cha mafanikio kwa wanamichezo” alisema Dkt. Mwakyembe.

Anazidi kueleza kuwa  Serikali itaendelea kuweka juhudi kwa timu za wanawake ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa katika michezo kwani zimekuwa zikifanya vizuri  ambapo ndani ya muda  wa miezi miwili zimeleta makombe mawili kutoka katika mashindano ya kimataifa ikiwemo  CECAFA.

Dkt. Harrison Mwakyembe alisisitiza kuwa zama za kupeleka wachezaji kwa mazoea zimepitwa na wakati bali wachezaji watakaokuwa wakishiriki michezo ya nje ya nchi ni wale wenye juhudi na uzalendo kwa taifa lao.

 Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Suzan Mlawi amezipongeza timu hizo na kueleza kuwa  Wizara imefanikiwa katika kuchagua wachezaji bora ambao wameiwakilisha vyema nchi na kuiletea heshima kubwa.

 “Haya ni mashindano ya kwanza kushiriki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na tumeweza kurejea na kombe tunahitaji pongezi sana, matokeo haya ya yanatokana na kupeleka timu zinazoweza kushindana”.alisema Bibi. Suzan

Awali akitoa mrejesho wa Mashindano hayo Mkuu wa msafara ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw. Addo Komba alieleza  kuwa Tanzania imeshiriki michezo minne ambayo ni Mpira wa Miguu wanawake,mpira wa pete,riadha pamoja na karate ambapo mpira wa miguu wanawake waliibuka washindi wa kwanza.





Mashindano hayo yameshirikisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Burundi ambao ndio walikuwa wenyeji,Tazania ,Kenya  Rwanda na Uganda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad