HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 12, 2018

WAHASIBU WATATU WA TTCL KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA WIZI WAKIWA WATUMISHI

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Wahasibu watatu wa shirika la Mawasiliano Tanzania, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za wizi wakiwa watumishi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh milioni 57.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita, amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Mercy Semwenda (49)  Flora Bwahawa (54) na Hawa Tabuyanja(54).

Mbele Hakimu Mkazi, Augustine  Rwizile imedaiwa, mshtakiwa Semwenda  peke yake anadaiwa, kati ya Januari Mosi mwaka 2017 na Septemba 21 mwaka 2017 jijini Dar es Salaam,  aliiba vocha za muda wa maongezi za TTCl zenye thamani ya sh 44,393,000/ pamoja na fedha za mauzo ya Vocha zenye thamani ya sh milioni 5,914000/

Imedaiwa kuwa, mshtakiwa alifanya uwizi huo kutokana na kamba alikuwa mfanyakazi wa TTCL kama Mhasibu.

Katika shtaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo, washtakiwa wote, waliisababishia Shirika la Mawasiliano  Tanzaniq, (TTCL), hasara ya sh. Milioni 57,773,122.

Hata hivyo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakamani hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi Mahakamani kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP

Kufuatia hivyo, kesi imeahirishwa hadi Julai 24.2018 kwa ajili ya kuja kutajwa, kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
 Wakili anayewatetea washtakiwa hao amedai, ingawa mashtaka dhidi ya washtakiwa hao yanadhamana lakini wameshtakiwa kwa sheria ya uhujumu uchumi, basi atafuata taratibu zote za kisheria kuomba dhaman Mahakama kuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad