HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 19, 2018

Ufuta wa wafanyabiashara uliokamatwa Kibiti kuuzwa kwa mnada

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Ufuta uliokamatwa Halmashauri ya Kibiti kutokana na kukosa nyaraka ya mnada kutoka Halmashauri ya Rufiji unapigwa mnada ikiwa ni agizo la serikali ya kutaka mazao ya Kahawa, Pamba na Ufuta kuuzwa kwa stakabadhi ghalani.

Uamuzi huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Gulam Hussein Kifu wakati wa kikao cha pamoja kati ya Halmashauri ya Kibiti na Rufiji wakiongozwa na wataalam Kutoka Wizara Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kifu alisema maamuzi ya kikao kuhusiana na ufuta uliokamatwa hauwezi kutenguliwa na mtu yeyote kutokana na Agizo la Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa kutaka mazao ya ufuta, Kahawa na pamba kwa mfumo wa Sitakabadhi Ghalani ili kuweza kumuinua Mkulima.

Amesema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kufuata utekelezaji wa maamuzi yanayotokana na serikali hivyo ufuta uliokamatwa upigwe mnada.

Kifu amesema kuwa hakuna mtu mwenye matatizo na wafanyabiashara isipokuwa ni kuwataka wafanyabiashara hao kufuata utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni.

Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kuwa baada ya ufuta kuuzwa kwa njia ya mnada watarudishiwa fedha zao walizonunulia ufuta kutokana na kilo zitakazouzwa.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo amesema kuwa maamuzi yaliyotolewa ni kutekeleza kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa mnada.

Hivi karibuni Mkurugenzi  Mtendaji wa  Halmashauri ya Kibiti, Alvera Ngabagoye aliwaambia waandishi wa habari  kuhusiana ufuta kukamatwa katika wilaya ya kibiti ikiwa ni kutekeleza agizo la serikali la kuuza katika mfumo wa stakabadhi ghalani  kwa kuhusisha mnada.
 Mkuu wa Wilaya ya Kibiti , Gulam Hussein Kifu akizungumza katika kikao cha pamoja kuhusiana na Ufuta uliokamatwa katika Wilaya ya Kibiti ukitokea Wilaya ya Rufiji na kumualiwa kuuzwa kwa njia ya mnada  
 Mkuu wa Wilaya ya Rufiji , Juma Njwayo akizungumza juu ya utekelaji wa agizo la kuuza ufuta kutoka kwa wakulima kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania wa Wizara ya Fedha na Mipango, Godfrey Malekano akizungumza kuhusiana na maamzu ya kikao kuhusiana na Ufuta.
Sehemu ya watendaji , wafanyabiashara pamoja na madiwani wa wilaya ya Rufiji waliokuwepo katika mkutano uliofanyika Kibiti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad