HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 23, 2018

MKUU WA MAFUNZO NA UTENDAJI WA KIVITA JWTZ AWATAKA ASKARI WAPYA 2,081 KUWA NA UTII, UAMINIFU NA UHODARI

Na Ripota Wetu, Arusha
MKUU wa Mafunzo na Utendaji wa kivita wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali Alfredy Kapinga amewataka askari wapya 2,081 kuhakikisha wanakuwa na utii, uaminifu na uhodari kwani huo ndio msingi wa jeshi.

Hayo aliyasema mjini Arusha wakati wa kufunga mafunzo ya kundi la 38 B la mwaka 2017 lenye askari wapatao 2,081 waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya kijeshi katika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha ambapo mafunzo hayo yalifungwa Juni 22, mwaka huu.

Akizungumza kwenye sherehe hizo Meja Jenerali Kapinga amewataka vijana hao kutambua tayari wameiva kuwa askari  na hivyo wapo tayari kutumika mahali popote na masuala ya longolongo kwa sasa hayapo tena.

“Jukumu kubwa mbele yenu ni kulinda nchi dhidi ya maadui wan je na ndani, kulinda mipaka na shughuli za kijamii mtakazokuwa mmepangiwa  endapo mtahitajika,” amesema Meja Jenerali Kapinga.

Katika hotuba yake hiyo amewataka pia wazazi nchini kuwaacha vijana hao wafanye kazi ya jeshi kwani wamekabidhiwa dhamana kubwa kwa taifa hivyo kitendo cha kuendelea kuwachukulia kama watoto si sahihi.

“Hawa tayari ni askari, tumewapokea tutawatunza na kuwafundisha maadili mema kwa taifa, ile mbereko ya kuwabeba sasa mziache hawa ni askari,” amesema Meja Jenerali Kapinga.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi Kihangaiko (RTS), iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani Kanali Sijaona Myala akizungumza kwenye sherehe hizo aliwataka wazazi kuacha kusikitika pindi watoto wao wanapopangwa kwenda nje ya nchi.

Naye Mkuu wa Kikosi cha 883 KJ Oljoro Luteni Kanali Christopher Kavalambi alisema miongoni mwa wahitmu hao wamo pia wanariadhara 10 na wanamichezo mingine ya mpira wa pete na ngumi.

Amewataja baadhi ya wanartiadhara waliomaliza mafunzo hayo ya awali ya kijeshi ni pamoja na Alphonce Simbu na Emmanuel Giniki.

Sherehe hizo za kuhitimu mafunzo zilishereheshwa na kwa gwaride  la kuhitimu mafunzo na maonyesho ya vikundi mbalimbali yaliyoandaliwa na kuruta waliohitimu mafunzo yao na kuwa askari.
 Askari wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakitoa heshima wakati wa Gwaride lao la kumaliza mafunzo ya wali ya kijeshi yaliyofanyika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha
 Askari wakionyesha moja ya maonyesho ya ukakamavu wakati wa kufunga mafunzo yao ya awali ya kijeshi yaliyofanyika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha jana 
Mkuu wa mafunzo na utendaji wa kivita Jeshini Meja Jenerali Alfredy Kapinga akikagua Gwaride la askari 2,081 la askari wapya wa JWTZ waliomaliza mafunzo yao Shule ya Mafunzo ya awali ya Kijeshi Kihangaiko (RTS), iliyoko wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo mafunzo hayo yalikuwa yakitolewa Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha.
 Askari wapya wakionyesha sarakasi wakati wa gwaride la kufunga mafunzo yao yaliyofanyika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad