HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 14 May 2018

TANZANIA YAINYUKA UINGEREZA YATINGA FAINALI MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA LA WATOTO

 Na Ripota Wetu, MJI WA MOSCOW ,URUSI 
MASHINDANO ya Kombe la Dunia la Watoto yameendelea tena katika Mji wa Moscow nchini Urusi ambapo Tanzania imefanikiwa kutinga fainali ya mashindano hayo baada ya kuifunga Uingereza mabao 2-1.

Mchezo huo ulichezwa katika Uwanja wa Klabu ya Lokomotive Moscow ambapo magoli ya Tanzania yalifungwa na mlinzi Mastura Fadhili na Mshambuliaji Asha Omari. 

Hivyo Tanzania itacheza fainali na Brazil kesho kutwa.Brazil waliibwaga timu ya Ufilipino katika nusu fainali goli 1-0.Magoli ya mechi zote yalifungwa kipindi cha pili huku Tanzania wakiumiliki mchezo kwa asilimia kubwa na watoto wa  kitanzania walionesha umahiri mkubwa sana mbele ya Mheshimiwa Balozi wetu na wa Tanzania nchini Urusi na pia maofisa wa Ubalozi wetu walihudhuria kutazama mechi hio. 

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Street Child United John Wroe ambao ndio  walioshiriki kuandaa mashindano haya alimpokea Balozi na ujumbe wake na kumpa zawadi na kisha baada ya mechi alimpa pongezi kwa ushindi uliopata Tanzania dhidi ya Uingereza. 

Timu ya Tanzania imefika fainali tena ikiwa imeruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu chini ya mlinda mlango mahiri Sifaeli Geofrey na pia Tanzania inaelekea kutetea taji lake fainali kwani ndio mabingwa wa kombe hili tangu yalipofanyika mashindano haya mwaka 2014 nchini Brazil. 

Hivyo kikubwa ni kuendelea kuiombea Tanzania ibebe tena kombe na tuendelee kuitangaza Tanzania Kimataifa zaidi. Mungu Ibariki Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad