HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 15, 2018

Standard Chartered wazindua michuano ya kuwania tiketi ya kwenda kuiona Liverpool

Na Mwandishi wetu
Benki ya Standard Chartered jana ilizindua awamu ya tatu  ya michuano ya soka ya kuwania kombe lake. Michuano hiyo ya kuwania kombe la Standard Chartered 2018 huchezwa kwa dakika 10 kila upande ukicheza kwa dakika 5. Michunao hiyo inasaka timu itakayoenda kushuhudia kipute kinachopigwa na timu ya Liverpoool. Hii ni mara ya tatu kwa michuano hiyo ya kusisimua kufanyika katika ardhi ya Tanzania kuanzia mwaka 2010.

The Standard Chartered Group ndio wadhamini wakubwa wa Liverpool Football Club kuanzia mwaka 2010 hadi  2018/2019. Kwa kushirikiana na klabu hiyo benki ya Standard huendesha mashindano ya soka ya dakika 10 katika masoko yake makubwa ya Bara la Asia, Afrika na Mashariki ya kati. 

Pia michuano hiyo inawezesha kuchangia katika kuendeleza soka. Ikiwa katika mwaka wake wa saba tangu kuanzishwa kwake katika masoko hayo, mashindano hayo yameendelea kuwa na nguvu zaidi kukiwa na washindi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia.

Kenya ilitwaa ushindi mwaka 2016, Korea kusini (2015), Vietnam (2014), Thailand (2013) na Singapore (2012). Michuano hiyo kwa kaiwada ina sehemu tatu kuanzia nchi wenyeji, kikanda na fainali zake hufanyika viwanda vya Anfield – Uingereza. Mwaka huu benki hiyo imebadili mfumo wa michuano na kwamba mshindi atapata tuzo na kwenda Anfield.

Akizungumza wakati wa uzinduzi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank nchini Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, alisema kwamba mwaka huu kutakuwa tofauti na kwamba mshindi wa mashindano ya ndani yenye timu 32 atatwaa kombe na  kwenda kuangalia mtanange wa ligi kuu ya England.

Timu zitakazoshiriki ni pamoja na wateja wa benki hiyo na michuano hiyo itaanza Juni 23 mwaka huu. Mwaka jana mashindano hayo yalikuwa ya kikanda ambapo timu kutoka Tanzania, Kenya na Uganda zilichuana vikali na timu ya Tanzania ya Azania – Mikoani Traders  walishinda na kwenda kwenye fainali Anfield.

Benki hiyo pia imesema itamleta mkongwe mwingine na nahodha wa Liverpool Sami Hyypia  mwaka huu na mwaka jana walimleta mkongwe John Barnes.

Sami atawasili nchini Juni 20 tayari kuhudhuria michuano hiyo na wakati akiwa nchini atakuwa na kliniki na timu ya Serengteti yenye umri chini ya miaka 17.Pia atakutana na vijana wenye mazingira hatarishi na watoto wenye akaunti katika benki  hiyo.

Bw.  Rughani pamoja na kusifu uhusiano wa benki hiyo na klabu ya Liverpool  pia amesema watakuwa na ushirikiano wa karibu na Shirikisho la soka nchini.

Naye Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi, alishukuru benki hiyo kwa kusaidia michezo hasa soka.

Alisema ana Imani kuwa timu hizo zitakazoshiriki zitapata nafasi ya kujifunza na kuondoka na kitu cha msingi katika uchezaji soka.


Watakaoipata nafasi ya kwenda Uingereza watapata nafasi ya kupata mafunzo yatakayotolewa na wakali wastaafu wa Liverpool na pia na kuona mchuano wa msimu wa timu hiyo katika ligi ya England.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akisalimiana na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo kabla ya mkutano na waandhishi wa habari kuhusu uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2018 mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba akitoa utambulisho kwa meza kuu wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia kwenda kushoto ni Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa Kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu, Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo, Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( wa pili kushoto) akizungumzia ziara ya nyota na nahodha wa zamani wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu akielezea kuhusu safari yao ya Anfield ambapo aliongeza na kusema amefurahishwa na msimu huu ambapo mashindano hayo hayashirikisha timu za nchi jirani wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo akizungumzia  ujio wa Hyypia ambapo alisema ni nafasi adhimu kwa timu yake kunolewa na nahodha huyo wakati wakijiandaa na mashindano ya mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana, katika mkutano na waandishi wa habari kwenye hafla fupi iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) ya uzinduzi wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (kulia) akitoa salamu za TFF ambapo aliipongeza benki ya Standard Chartered nchini kwa kuinua soka la Tanzania kimataifa kupitia mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa mashinano hayo zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba.
Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (wa kwanza kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( kushoto) wakizundua sanamu ya nyota na nahodha wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba ( wa kwanza kulia), Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu (wa pili kushoto) pamoja na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo (wa tatu kulia).
Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (wa kwanza kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( kushoto), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (wa kwanza kulia), Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu (wa pili kushoto) pamoja na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo (wa tatu kulia) wakipata picha ya ukumbusho baada ya kuzindua sanamu ya nyota na nahodha wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya waandishi wa habari na wadau wa michezo waliohudhuria wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi akipiga mpira huku akiwa amefungwa macho na kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018  wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akipiga mpira huku akiwa amefungwa macho na kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018  wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu akipiga mpira huku akiwa amefungwa macho na kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018  wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo akipiga mpira huku akiwa amefungwa macho na kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018  wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni ya Channel Ten, Said Makala akiwakilisha wanahabari wa michezo kupiga mpira akiwa amefungwa macho na kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018  wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Mwanaspoti la kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, (MCL), Imani Makongoro akiwakilisha sports ladies kupiga mpira akiwa amefungwa macho na kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018  wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akimkabidhi Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi zawadi ya begi la vifaa vya michezo mara baada ya kuhitimisha sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo, Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani pamoja na Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered nchini, Mariam Sezinga akimkabidhi zawadi Mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Mwanaspoti la kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, (MCL), Imani Makongoro mara baada ya kuhitimisha sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad