HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 14 May 2018

MIAKA 70 YA NAKBA YA WANANCHI WA PALESTINA

Taifa letu la Palestina  linaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 ya Nakba (janga), likiendeleza mapambano kabambe ya kurudisha haki zake thabiti za kizalendo, kuondoa athari na matokeo yake ambayo bado yapo katika nyanja zote za maisha ya taifa letu. Hiyo ni tangu utekaji wa ardhi yote ya Palestina ya kihistoria hadi kuwatoa nusu ya wananchi wa Palestina nje ya nchi yao. Kwa yakini mapambano ya kitaifa kwa ajili ya ukombozi yatathibitisha malengo yake hata kama ni kwa muda mrefu, licha ya uadui wa utekaji na uhalifu wake unaoendelea, na licha ya uungaji mkono wa Marekani uliopitiliza chini ya Rais wake Donald Trump kwa  taifa tekaji la Israel, hasa uamuzi wake wa kusikitisha wa kuizingatia Jeruselemu kuwa ni mji mkuu wa taifa tekaji na kuhamishia ubalozi wa Marekani mjini Jerusalemu, jambo linalokiuka  sheria ya kimataifa na maazimio yake, pia ni jambo linaloifanya Marekani kuunga mkono utekaji na uadui dhidi ya wananchi wa Palestina na suala lake la kizalendo.


Kama ilivyo kila mwaka tarehe 15 Mei, wananchi wetu popote pale walipo kwa nguvu za kizalendo na taasisi zake huikumbuka kumbukumbu hii yenye kuumiza kwa shughuli na harakati mbali mbali. Lakini mwaka huu unashuhudia mabadiliko makubwa na muhimu katika kuutukuza mnasaba huu, kwani inaenda sambamba na safari kubwa ya kurejea iliyoanza tangu wiki kadha kwenye mipaka ya kihistoria ya Palestina pamoja na ukanda wa Gaza.
 Makumi ya watu wamekufa mashahidi na maelfu wamejeruhiwa. Kilele chake kitakuwa tarehe 14 -15 Mei, hii kwa kuthibitisha wananchi wetu wameshikamana na malengo na haki zake za kizalendo na mbele kabisa haki yake ya kurudi vijijini kwao na mali zao; na haki ya kusimamisha taifa lake huru lenye heshima kamili katika mji wake mkuu Jeruselemu, pamoja na kuondolewa kuzingira kuovu katika ukanda wa Gaza.

Ukweli msimamo wa Marekani na hatua iliyoichukua mnamo Januari mwaka huu, wa kupunguza msaada wake kwa UNRWA kwa kiasi cha dola za kimarekani millioni 65 toka kile kiasi inachokitoa kwa UNRWA. Uamuzi huu kwa taifa letu umepelekea hofu kwa suala la wakimbizi kwa kujaribu kulifuta na kuliweka hatarini kwa masilahi ya msimamo mkali wa serikali ya Israel ambao unajitahidi kwa nguvu zote kulitokomeza suala la wakimbizi ambalo ndio kiini cha suala la Palestina. Hiyo ni kukausha vyanzo vya misaada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia na kuwahudumia wakimbizi wa Palestina (UNRWA), hadi kufikia kuliondoa kikamilifu.


Katika kumbukmbu ya 70 ya Nakba (janga) ya Palestina,majukumu yetu wote yanaongezeka kuhusiana na suala letu la haki,katika ulazima wakupambana na kukabiliana na maelezo ya kizayuni na kiizraeli kuhusu Nakba lililowakumba Wananchi wa Palestina, ambalo limepelekea kuhamishwa maelfu ya wapalestina, hasa kile kilichojumuishwa na “Mpango wa Dalet” uliopitishwa na Shirika la Kizayuni mwanzoni mwa mwaka 1948 na kuachiwa utekelezaji wake Haganah (kikundi cha mauaji na utesaji) kwa muongozo wa uwazi,kama vile kuua,kuhofisha,kuzingira miji na vijiji vya palestina,kuchoma nyumba na mali,kuzika mabomu katika vifusi ili kuwazuia wenyeji kurejea Kartika nyumba zao.

Vikundi vya hagana na jumuiya zingine za kizayuni kufuatia mpango huo zimetekeleza mauaji 28,huku mauaji mabaya zaidi katika hayo ni yale ya mjini Deir Yassin mnamo tarehe 9 April 1948. Hii ni pamoja na kuvunjwa na kuteketezwa miji na vijiji 531,kuhamishwa wapalestina laki nane (8) waliofanywa kuwa ni wakimbizi katika nchi yao, ni sawa waliokuwa katika ardhi ya mwaka 48,Ukingo wa Magharibi au Ukanda wa Gaza.


Tukiwa tunaadhimisha kumbukumbu ya Nakba (janga),ni vyema kutaja nyaraka na tafiti za kielimu, dalili za wazi zenye kuthibitisha ukweli wa maelezo ya Palestina na uongo wa maelezo ya kiisraeli,hususan nyaraka rasmi za Israeli zilizoonesha aliyoyasema Waziri Mkuu wa zamani wa Israeli amabe ni kiongozi wa chama cha Herut na baadae chama cha Likud, gaidi “Menachem Begin”, aliyesema: Lau si mji wa Deir Yassin (mauaji yaliyopoteza kiasi cha wapalestina320 waliokuwa karibu na Jerusalemu) isingekuwepo Israeli. 
Kama inavyowezekana kupata muongozo kupitia maandiko ya wanahistoria wengi wa Israeli waliokuwa maarufu,mfano “Ilan Pappe” kuhusu utokomezaji wa kikabila nchini Palestina, pia “Benny Morris” kuhusu ule mpango uliojulikana kwa jina la “Mpango wa Dalet”,kuwa ni uongo wa kuondoka kwa hiari kwa Wapalestina.
Hakika kutaja ukweli huu na kuweka wazi uovu wa vikundi vya kizayuni na dola ya Israeli na kuzionesha kwa ulimwengu mzima,hakulengi kuandika ukweli wa kihistoria tu kwa malengo ya kimaarifa na kinadharia, bali hilo ni jambo linalohudumia mpango wetu wa kitaifa na malengo ya mapambano yetu ya sasa,katika kudai haki na kuondoa dhulma kwa wananchi wa Palestina, pia kulaani ufashisti (udhalimu) na ubaguzi wa kizayuni.
 Pia kudhihirisha majukumu ya dola tekaji katokana na dhulma ya kihistoria dhidi ya wananchi wa Palestina,vilevile kutilia mkazo majukumu ya jamii ya kimataifa katika kukomesha dhulma na haki ya wananchi wetu ya kufikia katika ufumbuzi wa kisiasa unaowiana iliyopo katika misingi ya haki na maazimio ya kisheria ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad