HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 14 May 2018

JAMII YAASWA KUJENGA MISINGI BORA YA MALEZI YA WATOTO –NKINGA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JAMII imeaswa kujenga misingi imara ya malezi ya  watoto ili wasiweze kuishi maisha ya mitaani na ambayo yanasababisha kokosa haki za kupata elimu pamoja na malezi mengine.

Hayo ameyasema leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga wakati akizindua ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania, amesema kuwa sehemu salama ya kuishi watoto ni katika familia au jamii.

Amesema kuwa katika ripoti hiyo watoto wa kike wamekuwa wakionekana katika majira ya usiku wakijiuza huku watoto wakiume wanaonekana majira ya mchana na usiku.

Nkinga amesema kuwa serikali itafanyia kazi mapendekezo ya ripoti hiyo ili katika kuweza kuhakikisha watoto hao wanakwenda katika familia zao.

Amesema sababu zinazowafanya watoto kuishi na kufanya kazi mitaani  ni umasikini pamoja na ukatili wa kupindukia na kuamua baadhi ya watoto kutoroka katika familia zao na kuingia mitaani.

“Jamii iendelee  kuishi kwa amani na misingi bora katika malezi ya watoto katika kuhakikisha hawakimbilii mitaani kwa kuishi kwa kukosa chakula, elimu pamoja wengine kupoteza maisha kutokana na kupigwa “amesema Nkinga.

Ripoti hiyo inatoa matokeo ya utafiti wa watoto wenye umri kati ya miaka 0-18 ambao wanaishi mitaani na kufanya kazi katika miji sita nchini kwa hesabu wanaoishi usiku na mchana  kwa watoto wanaoishi mitaani na kufanya kazi wakati wa mchana 6,393 na usiku 1,385  kwa wavulana waliohesabiwa mchana ni asilimi 76 ya watoto wote  wasichana  walifikia asilimia 24 wakati mchana na usiku kwa wasichana iliongezeka na kufikia asilimia 30 wakijihusisha na ngono  huku asilimia hiyo ikipungua kwa asilimia 70 wakati wa usiku .

Mapendekezo ya ripoti hiyo ni kwa serikali na wadau wengine kuhakikisha kwamba watoto wanaoishi nakufanya kazi mitaani kuwaungnisha katika mifumo ya ulinzi wa watoto katika ngazi zote za kitaifa  na kiwilaya.

Mkurugenzi wa Railway Afrika, Peter Kent amesema kuwa kazi yao ni kutaka watoto kurudi katika familia zao na kuendelea kuishi huku wakiwa wanafatilia kuhakikisha haki za msingi wanazipata.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Railway Afrika, Peter Kent akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati ya shirika hilo katika masuala ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Mwakilishi Mkazi USAID Kizazi Kipya Project wa PACT Tanzania, Levina Kikoyo akizungumza jinsi ya utafiti waliofanya katika ripoti hiyo.
 Sehemu ya wadau mbalimbali wa masuala ya watoto waliohudguria katika uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga akiwa na wawakilishi wa mashirika wakati wa uzinduzi ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad