HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 18, 2018

Hospitali ya Dodoma yapewa miezi 8 kujenga mtambo wa kuteketeza taka

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola ameanza ziara ya kikazi ya siku saba katika Jiji la Dodoma kwa lengo la kukagua utekelezaji na uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira nchini.
Katika siku ya kwanza ya ziara yake Mhe. Lugola ametembelea Ofisi za Jiji na kupokea taarifa ya hali ya mazingira katika usimamizi wa Taka ngumu, taka za maji pamoja na madini ujenzi.
Akitoa taarifa ya Jiji Mkurugenzi Bw. Godwin Kunambi amesema kuwa Ofisi yake imepanga kujenga mabwawa makubwa ya maji taka katika eneo la Nzuguni na ujenzi wake uko mbioni kuanza.
Akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Kaimu Mganga Mkuu Mfawidhi  Dkt. Carolyne Damian amemueleza Naibu Waziri kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya mtambo wa kuteketezea taka.
Akiwa katika ziara hiyo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Dodoma kuhakikisha changamoto hiyo ya mtambo wakuteketeza taka unapatiwa ufumbuzi mapema ili kuhifadhi mazingira.
Aidha, Mhe. Lugola ametoa muda miezi nane kwa uongozi wa Hospitali hiyo  kuhakikisha mfumo wa matumizi ya kuni kama nishati ya kupikia unasitishwa na kuwataka watumie gesi ili kuhifadhi mazingira. 
Ziara ya Naibu Waziri katika Jiji la Dodoma inaendelea kwa kutembelea machinjio ya Punda Kizota na Mamchimbo ya Mchanga na Kokoto - Chogongwe.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akiwa na uongozi wa Hospitali ya Mkoa Dodoma mara baada ya kufanya ziara ya kikazi hospitalini hapo kukagua masuala ya taka ngumu na taka za maji na kuona uteketezaji wake. 
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akitoa maelezo kwa Bw. Carle Lyimo Afisa Afya Mkuu wa Jiji la Dodoma wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.
Mtambo wa kuteketeza taka ulipo katika Hospitali ya Dodoma ambao miundominu yake kwa sasa haukidhi mahitaji. Waziri Lugola autaka uongozi wa hospitali hiyo kuweka kipaumbele ujenzi wa mtambo huo mapema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad