BASATA yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania
Na
Mwandishi wetu
Baraza
la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza kampuni ya Compass Communications
Tanzania kwa kufanya mashindano bora ya Miss Universe hapa nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Mratibu wa mashindano
ya Miss Universe Fausta Magoti wakati wa kufanya tathimini ya mashindano ya
mwaka jana ambapo, Caroline Benard aliibuka mshindi.
Magoti
alisema kuwa pamoja na kampuni ya Compass kuanza kushiriki katika mashindano ya
Miss Universe mwaka 2007, waliweza kufanya vyema na kuitangaza Tanzania nje ya
mipaka yake.
Mbali
ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, Magoti alisema kuwa
wameridhishwa sana na utendaji wa kamati hiyo kwa kuteua majaji ambao wamekuwa
wakiwatangaza washindi ambao ni mfano bora kwa tabia kwa jamii.
“Washindi
wenu hawana kashfa katika jamii, mmeendesha mashindano yasiyokuwa na
malalamiko, kwa kwa kweli mnahitaji kupongezwa pamoja na kupata changamoto
nyingi kutoka kwa wadhamini,” alisema Magoti.
Alitoa
wito kwa waandaaji kupanua wigo wa mashindano yao na kuyafanya katika mikoa
mingi ili kujitangaza zaidi. “Najua changamoto kubwa ni kuapata wadhamini,
tunaomba mjitahidi ili kuyatangaza zaidi mashindano yenu, Basata tumeridhishwa
na utendaji wenu, tunataka mfanye bora zaidi ya hapa,” alisema.
Mrembo
Flaviana Matata ambaye alimaliza katika hatua ya sita bora katika fainali za
mashindano ya mwaka 2007, kwa sasa amekuwa akifanya vyema nje ya nchi katika
sekta ya maonyesho ya mavazi au wanaminitindo.
“Ni
mashindano bora ambayo kwa kweli yametuvutia sana, tunaomba muongeze bidii ili
kuyaboresha zaidi kwani mashindano haya kwa sasa ni makubwa na warembo wengi
wanayaulizia jinsi ya kujiunga nayo,” alisema.
Mkurugenzi
wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya
Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa mashindano
katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajiathidi kuongeza wigo wa
washiriki kaika mashindano ya mwaka huu.
Maria
alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo, bado wanahitaji
msaada kutoka Basata ili kupata wadhamini.
“Basata
ni chombo cha serikali, mnaweza kutusaidia kupata wadhamini hata kwa Wizara ya
Maliasili na Utalii, sisi tunatangaza jina la nchi na utalii pia, tunaamini
kupitia kwenu, tunaweza kupata sapoti kubwa kutoka wizara hiyo, Bodi ya Utalii
(TTB) na mamlaka ya zake kama Tanapa.

No comments:
Post a Comment