UPIGE MWINGI na Airtel – Kila mtu ni mshindi ukiwa na Airtel! - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 3, 2023

UPIGE MWINGI na Airtel – Kila mtu ni mshindi ukiwa na Airtel!

 

Dar es Salaam, Jumatano 3 Mei 2023: Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania ambayo inaongoza hapa nchini kwa kutoa huduma za mawasiliano pamoja na huduma za fedha kupitia simu za mkononi leo imetangaza kuzindua promosheni mpya kupitia huduma yake ya Airtel Money inayojulikana kama UPIGE MWINGI PROMO (KILA MTU NI MSHINDI) ambapo wateja watajishindia zawadi kambabe pale wanapofanya miamala kwa kutumia mtandao wa Airtel. Hii ni promosheni ya kipekee kwani kila mteja wa Airtel ni mshindi. Wateja wataweza kujishindia zawadi za hapo kwa papo kama vile muda wa maongezi, Pikipiki, TV, Friji na fedha taslimu kuanzia Tzs 1 milioni kila siku mpaka Tzs 50 milioni. N sio hivyo tu, kila siku sababu ya kutabasamu kwa wateja wa Airtel kwani sasa kuangalia salio la akaunti ya Airtel Money ni bure kwa wateja wote.

Kwenye promosheni hiyo ambayo itadumu kwa kipindi cha miezi mitatu, kila mteja wa Airtel anaponunua bando au kufanya muamala wowote kwa kutumia Airtel Money (Kama vile kutuma fedha, kutoa fedha, kulipa bili au Lipa namba) atapata zawadi ya papo kwa hapo ya muda wa maongezi na vile kuingia kwenye droo ya kila siku, wiki na ya mwezi na kujishindia zawadi. Mteja anayefanya miamala mingi zaidi anayo nafasi ya kubwa ya kujishindia zawadi. Mawakal wa Airtel Money wanayo nafasi ya kuingia kwenye droo na kujishindia zawadi pia.

Airtel kuanzia leo imetoa gharama za kuangalia salia. Mteja anaweza kupiga *150*60# au kutumia applikesheni ya Airtel, hakuna gharama tena kwa kuangalia salio. Airtel imekuwa Kampuni ya kwanza nchini Tanzania kutoa gharama za kuangalia salio la Airtel Money kwa wateja wote. Ukiwa na Airtel kila mtu ni mshindi!

Lengo la promosheni hii ni kuendelea kuhamashisha wateja na mawakala kutumia huduma za Airtel na wakati huo huo kupata nafasi ya kujishindia na Airtel na kuweza kutimiza ndoto zako. Kutakuwa na zawadi za kila siku ambapo washindi 90 watajishindia Tzs 1 milioni, washindi 48 wa kila wiki ambapo watajishindia friji la milango miwili na TV saizi 55’’, washindi wawili kujishindia pikipiki mpya kwenye droo ya mwezi na mshindi mmoja kujishindia Tsz 50 milioni kwenye droo ya mwisho.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua promosheni hiyo ya UPIGE MWINGI PROMO (KILA MTU NI MSHINDI), Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema ‘ Upige Mwingi na Airtel ni promosheni ya kipekee ambapo kila mteja wa Airtel kwa sasa atapata zaidi pale anakapotumia huduma za Airtel. Kila mtu atajishindia zawadi ya muda wa maongezi papo kwa hapo pale atakapokuwa amefanya muamala wowote au kununua bando. Vile vile, mteja atajishindia zawadi ya fedha taslimu ya Tzs 50 milioni. Promosheni hii ni moja ya mfano wa vile tunaongeza dhamana kwa kurudisha kwa wateja wetu na kuongeza hamasa jinsi ya kutumia Airtel Money kwa matumizi mbali mbali. Nawatakia kheri wateja wetu wote.

Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Andrew Rugamba aliongeza ‘Sisi Airtel, tunajali na tumejitolea kuhudumia na kudhamini wateja wetu. Airtel Tanzania ilikuwa Kampuni ya kwanza kuondoa tozo kwenye miamala ya simu kwa wateja wote na sasa ndio ya kwanza kuondoa gharama za kuangalia salio. Hii inaongeza dhamana kwa wateja kwa kila mteja wa Airtel Money na kuwafanya kuwa washindi.

Singano alielezea mipango ya Airtel ya kuendelea kusambaza huduma zake kote nchini. ‘Tumekuwa tukiendelea kupanua wingo wa mtandao wetu na mpaka sasa tuna Airtel Money Branches zaidi ya 3,500 na mawakala zaidi ya 200,000 huku pia tukiendelea kuwekeza kwenye kupanua mtandao wa 4G ili kufikia Watanzania wote na hasa kwa maeneo ya vijijini. Kwa kuendelea kupanua wingo wa mtandao wetu pamoja na huduma na bidhaa bunifu, wateja wetu wataendelea kufurahia huduma zetu za kipekee nchini kote. Na kwa promosheni hii ya Upige Mwingi na Airtel – Kila mteja wa Airtel ni mshindi.

Msanii wa maigizo ambaye ni Balozi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Lucas Mhavile maruufu kwa jina la Joti akizungumza na wakazi wa Mbagala Zakhen jijini Dar es Salaam wa uzinduzi wa promosheni ya UPIGE MWINGI na Airtel – Kila mtu ni mshindi ukiwa na Airtel. .Promosheni ya Upige Mwingi na Airtel ya kipekee kwani kila mteja au wakala wa Airtel wataweza kujishindia zawadi za hapo kwa papo kama vile muda wa maongezi, Pikipiki, TV, Friji na fedha taslimu kuanzia Tzs 1 milioni kila siku mpaka Milioni Tsh 50.
Mkurugenzi wa A irtel Mauzo Bw, Yusuph Kalufya akiongea na wakazi wa Mbagala jijini DSM katika viwanza vya Zakhem wakati wa kuzindua promosheni kabambe ya UPIGE MWINI na AIRTEL. itawawezesha wateja na wakala wake wote nchini kujishindia zawadi kambabe pale wanapotumia huduma au wanapofanya miamala kwa kutumia Airtel Money. Hii ni promosheni ya kipekee kwani kila mteja au wakala wa Airtel ni mshindi. Vilevile Airtel imetangaza kuondoa makato kwa kila mteja anapoangalia salio kupitia huduma ya Airtel money

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad