SIMBA WAWILI LUCY NA LIANA WATAKAVYOCHOCHEA UTALII WA NDANI SONGEA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 7, 2023

SIMBA WAWILI LUCY NA LIANA WATAKAVYOCHOCHEA UTALII WA NDANI SONGEA

 

 

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii imeleta simba wawili majike wanaitwa Lucy na Liana katika bustani ya wanyamapori
Ruhila Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ili kuchochea utalii wa
ndani.

Akizungumza kwenye hafla ya upokeaji wa simba hao iliyofanyika ndani ya bustani ya Ruhila mjini Songea, Mkuu wa Utalii kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda
ya Kusini Mashariki Kamishina Msaidizi Said Mshana amesema simba hao wametoka hifadhi ya wanyamapori ya Sevo jijini Arusha.

“Hawa simba kule sevo wildlife watu walikuwa wanapiga nao picha na kuwakumbatia ndiyo hawa,sasa sisi tukaona ngoja tuwalete Ruvuma na tumeamua wabaki kama simba ili kuchochea utalii wa ndani kwa watu wa Songea ambao kwa muda mrefu waliomba tuwaletee simba’’,alisema Kamishina Mshana.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Ndile ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea ameipongeza TAWA kwa kuleta simba hao katika bustani ya wanyamapori Ruhila ambapo amesema simba hao.

watawahamasisha wananchi kupenda kufanya utalii wa ndani, Amesema kuwa bustani hiyo ni kwa ajili ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na watanzania kwa ujumla ambapo amesema huo ni mkakati wa serikali ya Mkoa wa Ruvuma kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo amesema mji wa Songea sasa utachangamka katika sekta ya utalii.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano ameipongeza TAWA kwa kuleta Wanyama hao ambapo amesema sasa wananchi wa mji wa Songea wamepata sehemu maalum ya mapumziko hivyo ametoa rai kwa wananchi kumiminika katika bustani ya Ruhila.

Amesema mji wa Songea una bahati kwa kuwa na bustani ya asili ya wanyamapori ya Ruhila iliyopo katikati ya mji na kwamba serikali imeiboresha bustani hiyo ambayo hivi sasa ina wanyamapori wengi
wakiwemo simba,nyumbu,pofu na pundamilia.

Amesema Manispaa ya Songea imemuunga mkono mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha maeneo ya vivutio vya utalii ambapo amesema katika Manispaa ya Songea kuna vivutio
vingi vikiwemo bustani ya Ruhila,Makumbusho ya Taifa ya Majimaji na chanzo cha Mto Ruvuma kilichopo milima ya Matogoro.

Antony Masebe ni Kamanda wa Kituo Kidogo cha Kanda Kusini Mashariki amesema watalii wa ndani katika bustani ya wanyamapori Ruhila wanaendelea kuongezeka ambapo takwimu za mwaka huu
zinaonesha kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu jumla ya watalii 750 wametembelea bustani ya wanyamapori Ruhila.

Ametoa rai kwa wananchi wa Songea katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Pasaka kufika kufanya utalii wa ndani katika bustani hiyo ambayo hivi sasa ina wanyamapori wa kuvutia wakiwemo simba
pundamilia, pofu, kakakuona, kuro, swalapala, sungura, nyumbu,jamii ya nyani na ndege ambapo amesema bustani hiyo ina madhari ya kuvutia ikiwemo maeneo ya michezo ya watoto,maeneo mazuri ya kupigia picha na maeneo ya kuweka kambi kwa ajili ya utafiti.

Amekitaja kiingilio katika bustani hiyo kuwa ni shilingi 2,360 kwa mtu wa kuanzia umri wa miaka 18,chini ya miaka 17 ni shilingi 1180 na kwa Watoto chini ya miaka mitano wanaingia bure.

Bustani ya asili ya Ruhila ambayo ipo chini ya TAWA ilianzishwa mwaka 1973 na imekuwa inapokea watalii wa aina mbalimbali kutokandani ya nje ya nchi.


Simba wawili wanaoitwa Lucy na Liana ambao wametoka bustani ya Sevo mkoani Arusha na kuletwa katika bustani ya wanyamapori Ruhila Songea kwa lengo la kuamsha utalii katika mji wa Songea mkoani Ruvuma.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano akizu gumza kwenye hafla ya kukabidhi simba wawili kwenye bustani ya Ruhila mjini Songea.
Mkuu wa Utalii kutoka TAWA Kanda ya Kusini Mashariki Kamishina Msaidizi Said Mshana akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi simba hao iliyofanyika ndani ya bustani ya wanyamapori Luhira Songea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad