KINONDONI WAZINDUA NA KUKABIDHI NYARAKA ZA MPANGO WA USIMAMIZI KUKABILIANA NA MAJANGA,MAAFA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 1, 2023

KINONDONI WAZINDUA NA KUKABIDHI NYARAKA ZA MPANGO WA USIMAMIZI KUKABILIANA NA MAJANGA,MAAFA

 Na Mwandishi Wetu

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam imezindua na kukabidhi nyaraka za mpango wa usimamizi na mpango mkakati wa namna ambavyo watakabiliana na majanga pamoja na maafa kwenye Wilaya ya Kinondoni.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule wakati wa kuzindua na kukabidhi nyaraka za mpango huo ambapo ameeleza maeneo yaliyobainishwa kwenye nyaraka hizo ni majanga ya kweli na ambayo yamekuwa yanatokea mara kwa mara.

"Kuna wajibu wa kusoma nyaraka hizo kwa wale wote waliokabidhiwa na baadae kuchukua hatua za utekelezaji wa mipango ambayo wameiandaa kukabiliana na maafa na majanga mbalimbali katika Wilaya hiyo."

Kwa upande wake Mratibu wa Masuala ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Winfrida Ngowi amesema Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kinondoni kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) ilitekeleza mradi wa kuimarisha uwezo wa Wilaya kupunguza vihatarishi vya maafa na kujenga jamii stahimilivu dhidi ya majanga.

"Lengo la utekeleaji wa mradi huo ni pamoja na kuweka mgawanyo wa majukumu kwa wadau wote waliop na kuainisha rasilimali zilizopo na kuweka mikakati endelevu na ya muda mrefu ya kupunguza vihatarishi vya maafa ikiwa ni pamoja na kuandaa mikakati ya namna ya kuwajengea uwezo wananchi.

Aidha amesema katika utekelezaji wa mradi huo ilifanyika tathmini ya kubaini vihatarishi vya maafa, uwezekano wa kuathirika na uwezo wa jamii kuzuia, kujiandaa na kukabili maafa.

"Tathmini hii ilifanyika katika mitaa ambayo ni Mtaa wa msisiri A (Kata ya Mwananyamala), Mtaa wa Kigogo (Kata ya Kigogo) na Mtambani (Kata ya Mzimuni) na Mtaa wa Mkunduge (Kata ya Tandale). Vigezo vilivyotumika kuteua mitaa hiyo ni suala la kujirudia kwa maafa ya mafuriko katika mitaa hiyo,"amesema na kuongeza tathmini ilifanyika kwa siku tano kuanzia Machi 6 hadi Machi 10 mwaka huu.

Amefafanua tathmini ya vihatarishi vya maafa wilayani Kinondoni ilibaini majanga makuu yanayoikabili ni mafuriko na magonjwa ya mlipuko. Mengine yaliyotajwa ni ajali za barabarani na ajali za moto.

Pia baadhi ya miundombinu ya kutolea huduma muhimu kwa jamii kama vile elimu ipo katika maeneo yanayoweza kukumbwa na mafuriko.

"Tathimini alibaini wanawake, watoto, watu wenye ulemavu na wazee huathirika zaidi na maafa ikilinganishwa na makundi mengine katika jamii pia, jamii haina uelewa wa kutosha kuhusu hatua zinazoweza kuchukuliwa na mtu mmoja mmoja ili kupunguza vihatarishi vya maafa."

Wakati huo huo Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Triningile Mwakalukwa ametoa mwito kuwa mpango na mkakati wa kupunguza vihatarishi vya maafa ulioandaliwa uwe chachu ya ushirikishaji jamii na wadau, kujenga uelewa kwa jamii kuhusu usimamizi wa maafa, kuimarisha mfumo wa utoaji tahadhari ya awali, kujenga uwezo wa kuzuia, kupunguza madhara, na kujiandaa kukabiliana na maafa.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule akizindua nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo watakabiliana na Majanga na Maafa leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule akizindua nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo watakabiliana na Majanga na Maafa leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule akionesha baadhi nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo watakabiliana na Majanga na Maafa mara baada ya kuzindua nyaraka hizo leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule akimkabidhi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe.Songoro Mnyonge nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo watakabiliana na Majanga na Maafa mara baada ya kuzindua nyaraka hizo leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi.Hanifa Hamza nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo watakabiliana na Majanga na Maafa mara baada ya kuzindua nyaraka hizo leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule akimkabidhi Afisa wa Jeshi la Zimamoto Wilaya ya Kinondoni nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo Watakabiliana na Majanga na Maafa mara baada ya kuzindua nyaraka hizo leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule akikabidhi nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo Watakabiliana na Majanga na Maafa kwa Akari wa Polisi Wilaya ya Kinondoni leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule akikabidhi nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo Watakabiliana na Majanga na Maafa kwa Mwakilishi kutoka Red Cross Wilaya ya Kinondoni leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule akizungumza katika hafla ya uzinduzi na kukabidhi nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo Watakabiliana na Majanga na Maafa leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule akizungumza katika hafla ya uzinduzi na kukabidhi nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo Watakabiliana na Majanga na Maafa leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Triningile Mwakalukwa
akizungumza katika hafla ya uzinduzi na kukabidhi nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo Watakabiliana na Majanga na Maafa leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi.Hanifa Hamza akizungumza katika hafla ya uzinduzi na kukabidhi nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo Watakabiliana na Majanga na Maafa leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Masuala ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu , Bi.Winfrida Ngowi akizungumza katika hafla ya uzinduzi na kukabidhi nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo Watakabiliana na Majanga na Maafa leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa masuala ya Maafa katika Wilaya ya Kinondoni wakiwa katika hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo Watakabiliana na Majanga na Maafa leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa masuala ya maafa katika Wilaya ya Kinondoni mara baada ya kuzindua kukabidhi nyaraka za Mpango wa Usimamizi na Mpango Mkakati wa namna ambavyo Watakabiliana na Majanga na Maafa leo Machi 31,2023 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MMG)


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad