WADAU WA BIASHARA YA NYAMAPORI WAIOMBA SERIKALI KUSAIDIA BUCHA ZAO KUPATA NYAMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 8, 2023

WADAU WA BIASHARA YA NYAMAPORI WAIOMBA SERIKALI KUSAIDIA BUCHA ZAO KUPATA NYAMA

Na: Calvin Gwabara – Morogoro.

Pamoja na Serikali kuweka Sheria,Kanuni na miongozo ya ya ufanyaji wa biashara ya Nyama pori na nyara zake ili kusaidia kupunguza ujangili nchini lakini biashara hiyo bado haifanyiki vizuri miongoni mwa Wafanyabiashara wa mabucha ya nyama hizo nchini kutokana na kukosa
nyamapori hiyo kwenye mabucha yao.

Hayo yamebainishwa kwenye Warsha ya wadau wa biashara ya Nyama Porinchini iliyoitishwa na Watafiti wa mradi wa biashaara, maendeleo na mazingira TRADE Hub kwa lengo la kutoa matokeo ya tafiti zilizofanywa na mradi huo kwa wadau na kupokea maoni ya wadau hao katika kupata
matokeo mazuri ambayo yatasaidia nchi kupiga hatua kupitia biashara hiyo nchini.

Akifungua Warsha hiyo Kaimu Rasi wa Ndaki ya Uchumi Kilimo na stadi za Biashara Dkt. Zena Mpenda amesema Serikali mara kwa mara imekuwa ikitengeneza mazingira mazuri kupitia kanuni na miongozo hiyo ili kuwezesha jamii kunufaika na maliasili hiyo kupitia Nyama pori na nyara zake ili isaidie jamii kulinda maliasili na kupunguza ujangili.

“Biashara ya Wanyamapori imepitia katika changamoto kadhaa hasa katika upande wa biashara na usafirishaji wa mazao ya wanyamapori ikiwemo biashara ya wanyama hai pamoja na nyara zake na ninaamini washiriki wote mtakubaliana nami kuwa kumekuwa na matukio ya ujangili ambayo yamekuwa yakiendelea katika maeneo ya hifadhi za wanyamapori kwaajili ya kujipatia kitoweo wao wenyewe lakini pia kupata kipato lakini serikali kwa upande wake imekuwa ikiandaa mikakati,sheria,sera na miongozo
mbalimbali kukabiliana na changamoto za ujangili”, alisema Dkt. Zena.

Dkt. Zena amesema hivi karibuni Serikali iliandaa kanuni na sheria za urasimishaji wa uwindaji wa Wanayamapori na uuzaji wa Nyamapori na Nyara zake ya mwaka 2020 na kanuni inayoshughulikia nyara ya mwaka 2010 lengo kubwa likiwa ni kupunguza ujangili na jamii kunufaika na
maliasili hiyo.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwataka wadau hao kutoa mapendekezo na maoni ya mazuri kwa watafiti hao ili waweze kuja na matokeo ambayo yataisaidia serikali kuhakikisha kwamba biashara hizo hazisababishi ongezeko la uharibifu wa mazingira na upotevu wa baionuai.

Akizungumzia malengo ya warsha hiyo Prof. Pantaleo Munishi amesema kuwasilisha matokeo ya awali ya tafiti zilizofanywa na mradi huo kabla ya kuziwasilisha serikalini ili waweze kama wadau kutoa maoni na mapendekezo yao yatakayoasaidia serikali na wao wenyewe wanaofanya biashara hiyo kuwa endelevu.

Amesema katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambako alipita wakati wa utafiti huo kumeonekana kuwepo kwa shauku kubwa ja mii kupata nyama pori kwenye mabucha rasmi hivyo wao kama wafanya biashara na wadau ni wakati mzuri kwao kutoa maoni yao kuhusu changamoto wanazokutana nazo na nini kifanyike ili jamii ipate nyama na wao wafanye biashara yenye haki.

“Lakini naomba tufikie mahali tuzingatie masuala ya asili kwa maana ya mazingira lakini pia tuzingatie masuala ya kijamii pia kama njia moja wapo ya kufanya biashara zetu ili kufikia maendeleo endelevu ambayo yanahusisha watu, biashara na Mazingira asili ikizingatiwa kuwa Tanzania inaingia mikataba mingi ya kimataifa ambayo lazima ifutwe”, alibainisha Prof. Munishi.

Kwa upande wake mmoja wa wafanya biashara ya bucha ya nyamaporikutoka mkoani Katavi bwana Gilbert Kaswiza amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na mradi huo katika kuhakikisha na kusaidia jamii kunufaika na maliasili kwa kupata nyama na pia wafanya biashara kufanya biashara inayozingatia haki na kulinda maliasili hiyo.

Amesema changamoto kubwa ya kukosekana kwa nyama kwenye bucha zao kunatokana na kutokuwepo kwa utaratibu mzuri wa upatikanaji wanyama pori hiyo na kuwafanya kutegemea nyama inayotokana na kupigwa kwa wanyama waharibifu kwenye vijiji kwa utaratibu wa wizara kitu ambacho kinafanya mabucha yao kukaa hata miazi sita bila nyama kutokana na kutokuwepo kwa mnyama mharibifu.

“Hii hali inaturudisha nyuma sana sisi kama watanzania ambao tumeamua kuwekekeza fedha nyingi katika uanzishwaji wa biashara hii na kufungua mabucha ya nyama pori maana tunalipia leseni na vibali vyote wengine zinafika hata milioni 70 tumekopa bank kufanya biashara hii lakini unakaa miezi sita huna nyama buchani inatuuumiza sana”, alieleza bwana Kaswiza.

Aidha ameiomba serikali kutathimini upya biashara hiyo na kusaidia kuweka utaratibu mzuri ambao utawezesha bucha zao kupata nyama pori na jamii kunufaika na rasilimali hiyo kupitia biashara rasmi na yenye haki ambayo inasaidia kupunguza ujangili katika hifadhi za taifa.

Mradi wa Utafiti wa Biashara,Maendelo na Mazingira (TRADE Hub)ni mradi wa miaka mitano unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na washirika wengine kutoka katika nchi kumi na tano za Afrika, Asia, Uingereza na Brazil kuanzia Februari 2019
hadi Machi 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad