MARIAM ULEGA AHAMASISHA WANAWAKE KUJITOKEZA UWANJA WA UHURU KUMPONGEZA MH. RAIS DK. SAMIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 17, 2023

MARIAM ULEGA AHAMASISHA WANAWAKE KUJITOKEZA UWANJA WA UHURU KUMPONGEZA MH. RAIS DK. SAMIA

 

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mariam Ulega amewahamasisha wanawake wote kuhakikisha Machi 19 mwaka huu wanajitokeza kwa wingi Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Dk.Samia Machi 19 mwaka huu atakuwa anatimiza miaka miwili tangu aingie madarakani kuwatumikia Watanzania, hivyo kumekuwepo na hamasa kutoka kwa viongozi na wananchi wakihamasisha kuitumia siku hiyo kumpongeza Rais kwa kazi nzuri anayoifanya ndani ya Taifa la Tanzania.

Akizungumza wilayani Kibaha mkoani Pwani Mariam Ulega amesema wamefika kwenye wilaya hiyo kuzungumza na jumuiya ya UWT ili kuhamasisha kujitokeza kwa wingi Machi 19 mwaka huu kumpongeza Rais.

“Tunafahamu Rais Samia amefanya mambo mengi katika nchi yetu ya Tanzania kwa kipindi kifupi cha miaka miwili, tuna imani naye , tunampenda sana. Rais amekuwa halali asubuhi, mchana, jioni amekuwa akitafuta fedha ili zitunufaishe watanzania lakini hasa wanawake

“Tunaona miradi mingi imetekelezeka kwa kipindi kifupi cha urais wake, ndugu zangu nawaombeni tujitokeze kwa wingi, sio lazima kuvaa sare , sisi wanawake ni wazuri na warembo, tukivaa nguo zetu za nyumbani pia tunapendeza,”amesema Mariam Ulega.

Amesisitiza kutokana na umuhimu wa siku hiyo ya Machi 19, viongozi wao UWT Taifa wamechukua jukumu la kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na siku hiyo itakuwa ni hatari pale Uwanja wa Uhuru.

“Kwa hiyo niwaombe twende kwa umoja wetu na nguvu zetu lakini pia tusiwaache waume zetu , tuhakikishe tunakwenda nao ,mimi Mheshimiwa Ulega nitamvalisha shati safi na muelekeo ni mmoja tu Uhuru.”No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad