MAKAMU MWENYEKITI UWT AIHIMIZA USHIRIKIANO KUKOMESHA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 8, 2023

MAKAMU MWENYEKITI UWT AIHIMIZA USHIRIKIANO KUKOMESHA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

 

Na Mwandishi Wetu Michuzi TV

MAKAMU Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Zainabu Shomari amesema jamii ya Watanzania inapaswa kushirikiana kukabiliana na changamoto zinazosababisha ukatili wa kijinsia ikiwemo kuwafichua wote wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Ametoa kauli hiyo wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati wa Kongamano la Wanawake katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inayofanyika kila Machi 8 ya kila mwaka ,hivyo amesema ili kukabiliana a ukatili wa kijinsia kwenye jamii,ni vema kukawa na ushirikiano wa kuibua matukio hayo ili wahusika wachukuliwe hatua.
Pia amesisitiza Watanzania wakishirikiana kwa pamoja kuwafichua wenye lengo baya la kuharibu kizazi kijacho cha taifa hili kwani wao ni maadui na wanapaswa kupigwa vita.

"Wafichaji wakubwa wa taarifa hizi ni wakina mama kwa sababu wanaofanya vitendo vya ukatili wa kijinsia ni ndugu wakaribu ,unaweza kukuta anayefanya wakati mwingine ni Mjomba, baba wa kufikia, kaka au wageni wanaokuja nyumbani.Hivyo mama akisema anahisi ndoa itavunjika au atavunja udugu."
Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa Wizara husika,vyombo vya ulinzi na usalama,vyombo vya dini na jamii kushirikiana kwa pamoja ili kuangamiza tabia za aina hiyo ambazo kimsingi zinapaswa kukemewa kwa nguvu zote.
Makamu Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa iko haja ya sheria kuongezewa ukali kwa wanaojihusisha na vitendo vya ubakaji na ikiwezekana wanaofanya hivyo wahasiwe na hivyo kukomesha kabisa vitendo hivyo.
Akizungumza zaidi kwenye Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani inayosema Ubunifu na mabadiliko ya technolojia,chachu katika kuleta usawa wa kjinsia ,hivyo amewashauri wanawake kutumia Teknolojia vizuri katika kukuza uchumi ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko kwa ajili ya biasahara zao.
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga,Abdala Ulega amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumapatia nafasi hiyo ambapo alielezea mambo ambayo Wizara yake imefanya kwa lengo la kuwainua wanawake wa Mkuranga.

"Awali nilikuwa naibu waziri wa wizara hii na tumefanya mambo mengi ikiwemo kuunda vikundi vya ufugaji, na uvuvi kwa kuwapatia kinamama majokofu ya kuifadhia samaki wasiharibike pamoja na kutoa mbegu bora ya ng'ombe wa kisasa ili kuwawezesha kiuchumi."No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad