WAZIRI GWAJIMA AZINDUA TAMASHA LA ZIFIUKUKI WASANII 50 WAJIPANGA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 15, 2023

WAZIRI GWAJIMA AZINDUA TAMASHA LA ZIFIUKUKI WASANII 50 WAJIPANGA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI

 

 Na Khadija Seif,  Michuzi

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi maalumu Dkt.Dorothy Gwajima amezindua rasmi Tamasha la Wadau wa Maendeleo Lengo likiwa ni Kuelimisha jamii juu ya fursa za Maendeleo ya kiuchumi kupitia Makundi maalum na kuwakumbusha wazazi na walezi maadili mema katika malezi na makuzi ya watoto.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Tamasha hilo lililopewa jina la " Zifiukuki" WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi maalumu Dkt.Dorothy Gwajima amesema Mojawapo ya jukumu la Wizara yake ni Kushirikiana na wadau mbalimbali kuelimisha Jamii, kufahamu,kutambua na kutumia fursa za kujiletea Maendeleo.

"Serikali na wadau wake imeendelea kufanya juhudi kuhakikisha wananchi wanapata elimu na ufahamu juu ya uwepo wa fursa za Maendeleo na umuhimu wa kupambana na kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwemo ule wa kiuchumi na ukatili kwa watoto."

Gwajima ameeleza kuwa bado ufatiliaji unaonesha wapo wananchi hasa wa Makundi ya wanawa,wajane,wazee na wengine wenye mahitaji maalum ambapo elimu haijawafikia kikamilifu.

"Kuzingatia mwitikio mkubwa wa wadau wizara imeona umuhimu wa jukwaa la pamoja la wadau wote wa maendeleo ili kuhunganisha nguvu ya kuhamasisha mwamko wa jamii kutambua fursa za kiuchumi sambamba na kukataa ukatili kwa watoto kama kampeni ya wizara ya Twende pamoja ukatili sasa Basi"

Pia meongeza kuwa kupitia tamasha hilo sehemu kubwa ya jamii itazidi kuelimika na kufahamu kuhusu uwepo wa mikopo bila riba kwa makundi maalumu, huduma za mikopo mbalimbali kwa riba nafuu na huduma mbalimbali kwa maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi Fagdi yenye Mabalozi wa Kupinga Ukatili Saimon Mpagatwa amesema taasisi hiyo ina wasanii 50 na zaidi pamoja na wadau mbalimbali wa Maendeleo nia ni kutekeleza Kampeni ya "Twende Pamoja ukatili Tanzania basi."

''Jukwaa hili limeundwa kuongeza nguvu na ndio utanzania kwamba jamii kwa hiari yake inasikiliza mipango ya Serikali kisha wanasema na sisi jamii tupo na Serikali kwenye jambo hili na kuwa kikosi kazi chenye lengo moja."

Aidha Mpagatwa amesema Tamasha hilo la "Zifiukuki " litakuwa na lengo la Kuhakikisha elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia na kwa watoto inatolewa pamoja a kueleza fursa zinazopatikana na kuwafikia watu wa maeneo mbalimbali.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia ,Wanawake na Makundi maalumu Dkt.Dorothy Gwajima pichani akiwa na wadau mbalimbali wa Kupinga Ukatili wakati akizindua Tamasha la "Zifiukuki " linalotarajiwa kufanyika April 27,28,29 mwaka huu Viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad