KONGAMANO LA WADAU WA GESI YA LPG AFRIKA MASHARIKI WADAU WA GESI WAKUTANA KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 9, 2023

KONGAMANO LA WADAU WA GESI YA LPG AFRIKA MASHARIKI WADAU WA GESI WAKUTANA KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

 

Dar es Salaam, Machi 8, 2023: Kongamano la Wadau wa Gesi ya LPG Afrika Mashariki 2023 ni tukio kubwa kuliko matukio yote katika sekta hii kikanda ambalo litawaleta wadau mbalimbali kutoka nchi zaidi ya 30 ambao watashiriki katika mkutano na maonesho maalum tarehe 15 hadi 16 Machi, 2023 katika Hoteli ya Kimataifa ya Johari Rotana kwa udhamini wa Oryx Energies na Sygma Cylinders. Kongamano hili limeungwa mkono na Wizara ya Nishati na taasisi ya EWURA pamoja na taasisi World LPG Association iliyoko jijijni Paris France.

Kongamano la Wadau wa Gesi ya LPG Afrika Mashariki pia litakuwa jukwaa litakalotumika kuweka kumbukumbu muhimu ya kuzinduliwa kwa Muungano wa Wadau wa LPG nchini Tanzania mnamo jioni ya tarehe 15 Machi katika Hoteli ya Kimataifa ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Mhe. January Makamba atakuwa mgeni rasmi katika tukio hili muhimu ambapo wadau wa ndani na nje ya nchi watakutanika kuzungumzia masuala mbalimbali nyeti yanayoikabili sekta hii katika kanda ya Afrika Mashariki, kuonyesha bidhaa zao, kuchochea uwekezaji na mahusiano mazuri. 

Aidha, ndani ya kongamano hili, Oryx Energies inaendeleza jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kudhamini Warsha ya WLPGA Good Industry Practices and Cooking For Life itakayofanyika tarehe 14 Machi. Washiriki wa warsha hii watapata fursa ya kufahamu mipango ya matumizi ya gesi ya LPG nchini Tanzania na mikakati mbalimbali ya kukabiliana na vikwazo vikuu vinavyokwamisha safari kuelekea matumizi ya nishati safi na salama zaidi ya kupikia.

Likiwa na wazungumzaji wenye weledi pamoja, majopo ya majadiliano na bidhaa na huduma mbalimbali kwenye maonesho, Kongamano la Wadau wa Gesi ya LPG Afrika Mashariki – Tanzania 2023 ni fursa nzuri ya kupanua uelewa na kupata ufumbuzi kwa wadau wa biashara katika sekta hii.

Kwa taarifa zaidi na kwa ajili ya kujisajili tembelea 
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania LPG Association, Amos Mwansumbue (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa kutangaza maonesho ya gesi ya kupikia (LPG EXPO Afrika Mashariki 2023) yanayotarajiwa kufanyika tarehe 15 hadi 16 mwezi huu kwenye hotel ya  Rotana jijini Dar es salaam. Kulia ni Catherine Ho, Mkurugenzi Mkuu wa LPG EXPO ambao ndio waandaaji wa maonesho hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa LPG EXPO,Catherine Ho akizungumza.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad