JUKWAA LA WANAWAKE MKOA PWANI WATOA PONGEZI KWA RAIS SAMIA, MARIAM ULEGA ATOA NENO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 12, 2023

JUKWAA LA WANAWAKE MKOA PWANI WATOA PONGEZI KWA RAIS SAMIA, MARIAM ULEGA ATOA NENO

 

Na Mwandishi Wetu Michuzi TV - Pwani

JUKWAA la Wanawake Mkoa wa Pwani umetoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa malezi yake mazuri kwa majukwaa hayo na wao wanajivunia uwepo wa Rais Samia.

Akizungumzia wakati wa Kongamano la Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani Mwenyekiti wa Jukwaa mkoani hapa,Mariam Ulega amesema wanajivunia kuwa na Rais Samia ambaye ndiye mwanzilishi wa majukwaa yote Tanzania.

"Binafsi na Wanawake wa Mkoa wa Pwani ambao tuko kwenye jukwaaa hili tunajivunia kuwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan ,majukwaa haya ambayo tunajivunia nayo yeye ndio mwanzilishi wake, amekuwa mfano wa kuigwa kwetu, hakika tutaendelea kumuunga mkono na kumpigania."

Aidha Mwenyekiti huyo ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakari Kunenge,Wabunge wa Viti Maalum, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani kwa namna ambavyo wamekuwa wakitoa kila aina ya ushirikiano kwa Jukwaa hilo ambalo leo limefika hapo lilipo.

Katika hatua nyingine Mariam Ulega amesema ataendelea kushirikiana na Wanawake wote wa Mkoa wa Pwani kwa kuhakikisha wanapata maendeleo huku akielezea umuhimu wa wanawake hao kuchangamkia mikopo inayotolewa na Halmashauri kwani ni mikopo isiyo na riba..

Akiendelea kuzungumza kwenye Kongamano hilo,Mariam Ulega amesema katika kumsaidia mwanamke wa Mkoa wa Pwani wameanzisha Kampuni ya Gomama ili kuwezesha kiuchumi Wanawake na hivyo amewaomba wajiunge kwa kununua hisa.Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani,Mariam Ulega akizungumza wakati wa Kongamano la Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani,Mariam Ulega (katikati) akiwa katika picha ya Pamaoja na Wanawake wa mkoa wa Pwani.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad