WAGANGA WAKUU HAMASISHENI MATONE YA VITAMINI A KWA WATOTO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 2, 2023

WAGANGA WAKUU HAMASISHENI MATONE YA VITAMINI A KWA WATOTO

 

Waganga Wakuu wa Halmashauri zote  nchini wamehimizwa  kuhamasisha utolewaji wa  matone ya vitamin A kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Hatua hiyo itasaidia kuimarisha kinga ya mwili na kuzuia vifo vya watoto chini ya miaka mitano vinavyosababishwa na ulaji duni wa vyakula mchanganyiko.

Rai hiyo imetolewa Februari mosi, 2023 na Afisa Lishe kutoka OR-TAMISEMI, Bi. Asiatu Mbwambo wakati wa kikao kazi cha  timu ya usimamizi shirikishi  kutoka OR-TAMISEMI   na watoa huduma wa kituo cha afya Matemanga kilichopo wilayani Tunduru.

Alisema msingi wa lishe unaitaka watoto chini ya miaka mitano kula vyakula mchanganyiko lakini milo ambayo wanapewa watoto haikidhu makundi matano ya vyakula.

" Watoto wanatakiwa kula vyakula mchanganyiko lakini milo yetu haikidhi aina ya vyakula kutoka makundi matano ya vyakula kwa hiyo  matone ya vitamin A yana vitamins  zinazosaidia kuboresha afya  na kuimarisha ukuaji wa mtoto."

" Upungufu wa Vitamini A mwilini unaweza kusababishwa na uwepo wa maradhi ingawa sababu kuu ni ulaji wa vyakula visivyo na Vitamini A ya kutosha," amesema Mbwambo

Amesema  kuwa utolewaji wa matone ya Vitamini A kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuboresha afya za watoto baada ya tafiti kuonesha kwamba upungufu wa Vitamini A kwa watoto huchangiwa pia na hao ulaji duni.

Mbwambo alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wazazi na walezi wote wenye watoto walio chini ya miaka mitano kuhakikisha wanawapeleka watoto kupata matone ya Vitamini A  katika kampeni zinazofanyika kila mwezi Juni na Desemba nchi nzima. 

Amesema ni muhimu sana  wazazi au walezi kuzingatia ulishaji wa  vyakula mchanganyiko kutoka makundi matano ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kuwapatia watoto virutubisho vya kutosha na kuwawezesha watoto kukua vizuri kimwili na kiakili.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad