WACHOMA MAHINDI MAARUFU MLIMA KITONGA WAMUANGUKIA RAISI SAMIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 17, 2023

WACHOMA MAHINDI MAARUFU MLIMA KITONGA WAMUANGUKIA RAISI SAMIA

 

Wafanya biashara hususani wauzaji na wachoma Mahindi mabichi kwenye
eneo maarufu la Mlima Kitonga Mkoani Iringa wamuomba Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
kupitia Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji na Mkuu wa
Mkoa huo Mhe. Halima Dendego kuona uwezekano wa kuwajengea
vibanda maalumu vya kufanyia biashara katika eneo hilo ili kuweza
kufanya biashara hiyo vizuri kwa msimu wa Mvua na Kiangazi na kujipatia
kipato cha kunedesha familia zao.

Wakiongea na SUAMEDIA katika eneo hilo Mmoja wa wafanyabaishara
hao bwana Yackonia Monyi wamesema eneo hilo ni moja kati ya maeneo
maarufu sana kwa Wasafiri wanapitia njia hiyo kwenda mikoa yote ya
nyanda za juu kusini kusimama na kuburudika kwa kununua mahindi fresh
kutoka shambani tofauti na maeneo mengine ambayo wanauza mahindi
yaliyokaa hata wiki na kupoteza ladha.

“Ndugu Waandishi hapa ni sehemu ya mapunziko kwa wanaumaliza
kupanda mlima huu mkali na maandalizi ya moyo ya wanaoshusha mlima
huu mkali,kwahiyo wanakula mahindi choma fresh kabisa na kununua na
bidhaa kama zawadi za kupeleka wanapokwenda na nikuhakikishie hapa
wanasimama Mwaziri,Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Mabalozi na
viongozi wengne wakubwa Serikalini lakini mazingira ya hapa ni mabaya
sana nyakati za mvua watu wanashindwa kusimama na sisi biashara
inakuwa ngumu sana na wateja wanakosa kula mahindi na vitu vingine,
tuombe Rais wetu mama yetu Dkt. Samia atusaidie na sisi maana Mzee
wetu Magufuli aliwajengea wale wa Dakawa kule Morogoro” alisema bwana
Monyi.

Nae kwa upande wake bwana Meddy Magubika Amesema hilo limekuwa
eneo maarufu zaidi kwa uchomaji wa mahindi yasiyo lala na matamu ndio
maana yanasimama magari makubwa na madogo n ahata mabasi ili
kuwapa nafasi wasafiri wao kula mahindi mazuri na kuendelea na safari.
“Hapa kwetu tunaamka usiku sana kuingia shambani kuvuna mahindi haya
mabichi na ikifika saa moja asubuhi unakuta tayari tushafika na watu
wanakula mahindi ya kuchoma na wengune wanabeba kwaajili ya kupeleka
zawadi majumbani kwao, hapa mahindi yasiyoalala hatuuzi kwakuwa
tunalinda soko letu lisiharibike ili tunaedelee kupata soko na kubaki na
umaarufu wetu” alieleza bwana Magubika.

Aliongeza “Kila mtu anayeanza safari kupita njia hii kwenda Njombe,
Songea, Mbeya, Tunduma, Katavi, Rukwa awe dereva wa magari makubwa,
mabasi, magari madogo na wanautumia usafiri binafasi anayejua eneo hili
lazima awaze kula mahindi ya kuchoma katika eneo hili sasa akipita wakati
mvua inanyesha kubwa hawezi kufungua dirisha kuchukua mahindi wala
kushuka na kwa maana hiyo sisi tunapoteza hela mahindi yanabaki
tunatupa na kupata hasara”.

Nae Mfanyabishara mwingine bwana Kasian Yuda amesema biashara ya
mahindi wanayoifanya inawasaidia katika kumudu mahitaji mbalimbali ya
familia zao kama vile kusomesha watoto, kujenga nyumba na mahitaji
mengine ya binadamu hivyo biashara hiyo wao wanaiona kuwa ni kazi
rasmi katika maisha yao kwakuwa wengine wameianza miaka mingi na
maisha yanakwenda.

“Unavyotuona hapa sisi wengine tumeridhi kazi hii hapahapa kwa wazazi
wetu, tunachoma mahindi na kuuza maana sio kila mtu lazima awe
mkulima wengine hatulimi lakini tunasaidia wakulima kupata soko la
mazao yao kwahiyo tunategemeana wao wanapata hela na sisi tunapata
kwa kuuza mazao yao na kuendeleza maisha yetu kwahiyo serikali
ituangalie sisi kama vijana tulioamua kujiajiri katika kilimo kwa njia hii”
alisema bwana Yuda.

Aidha wameomba eneo hilo kuboreshwa kwa maana ya kuongezewa pia
nafasi au kuhamishiwa sehemu nzuri kuwezesha magari mengi zaidi
kusimama na kupata huduma kwakuwa eneo hilo ni dogo na hufika wakati
magari mengine hushindwa kusimama kwakuwa panakuwa pamejaa na
hawawezi kusimama katikati ya barabara kutokana na eneo hilo kuwa
hatari kwa magari yanayopita kushuka au kumaliza kupanda mlima huo
mkali.

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan amekuwa akihimiza vijana wengi kujiajiri katika kilimo kwa kuingia
katika mnyororo wa thamani kama ambavyo vijana hao wamefanya hivyo
kilio chao kikisiwa na kutatuliwa kitasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa
vijana kwenye eneo hilo maarufu kwa uchomaji wa mahindi mabichi nchini
na kuongea usalama kwa abiria na abiria wanaosimama eneo hilo kulamahindi mabichi kutoka sahambani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad