SUA YAJIVUNIA MATOKEO YA UTAFITI WA MRADI WA GRILI KATIKA KUBORESHA TIBA ASILI NCHINI. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 1, 2023

SUA YAJIVUNIA MATOKEO YA UTAFITI WA MRADI WA GRILI KATIKA KUBORESHA TIBA ASILI NCHINI.

 

Na: Amina Hezron – Njombe.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)

Upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Walad
Mwatawala amepongeza Watafiti wa Mradi wa GRILI kwa kufanikiwa
kufikia malengo yote matatu ya utafiti huo muhimu kwa Taifa.

Pongezi hizo amezitoa wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwisho wa
Mradi huo unaofanyika mkoani Njombe na kuwakutanisha wadau wote wa
mradi kutoka ndani na nje ya nchi kupokea matokeo ya mwisho ya Mradi
kutoka kwa wasimamizi wa Mradi huo na Wanafunzi waliokuwa
wanasomeshwa na mradi wakifanya tafiti mbalimbali.

“Sisi kama Chuo tumefurahishwa na utekelezaji wa mradi huu ambao
ulikuwa na malengo makuu matatu ya kujenga uwezo na tutaona hapa
waliyoyafanya, Kuzalisha elimu mpya pamoja na mifumo mipya ya
biashara kwenye eneo la mimea dawa ambayo ni muhimu kwa uchumi wa
wadau kwenye mnyororo wa thamani wa mimea dawa nchini” alisema Prof.
Mwatawala.

Aidha amesema kama Chuo wamefarijika kuona mradi umezalisha
Wanafunzi watano (5) wa Shahada ya uzamivu kwenye masuala ya Mimea
dawa na saba (7) wa shahada ya uzamili ambao kwa ujumla wameweza
kuzalisha machapoisho ya kisayasi 17 kwenye eneo hilo muhimu huku
akitumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa mradi huo Prof. Faith Mabiki
kwa kazi kubwa aliyoifanya na wasimamizi wengine wa mradi huo ambao
anaamini katika kipindi kifupi machapisho hayo ndiyo yamemuwezesha
kupanda cheo kutoka Udaktari na kuwa Profesa.

Amesema mfumo mzuri wa biashara ya bidhaa za mimea dawa
uliotengenezwa na Mradi huo utakuwa kichocheo kizuri cha mabadiliko na
mafanikio ya biashara ya dawa asili kwakuwa anatambua dawa hizo
zinauzwa kila kona nchini na watu wanazitumia lakini sasa kwa mfumo huu
zitaweza kuuzwa katika mifumo rasmi.

“Kitu kingine muhimu ambacho ni kizuri mradi huu umefanya ni
kuwaunganisha wadau wote kwenye mnyororo wa thamani wa bidhaa za
mimea dawa kupitia Jukwaa lake la Ubunifu wa bidhaa zitokanazo na
mimea dawa (GRIP) ambalo limesaidia kuwaweka pamoja wadau wote na
kujadiliana maendeleo na changamoto na kuzitatua kwa pamoja ambalo
linasimamiwa na SUA lakini wazo lilitoka kwenye mradi huu wa GRILI”
alipongeza Prof. Mwatawala.

Akizungumza malengo na mafanikio ya Utafiti Mkuu wa Mradi huo Prof.
Faith Mabiki amesema mradi ulijikita katika kushughulika na bidhaa
zitokanazo na mimea dawa kwa maana ya tiba asili na mnyororo mzima wa
thamani ili kusaidia Tanzania kunufaika na utajiri mkubwa ilionao wa
maliasili hususani mimea dawa kwa kufikia soko la Dunia.
Aidha amesema utafiti huo ulilenga kusaidia Tanzania kufikia mpango
wake wa maendeleo endelevu wa 2025 unaotambua mchango wa matumizi
ya maliasili ikiweo mimea dawa ambayo ipo nchini na inatumiwa lakini
haijaweza kushika vyema Soko la ndani na kimataifa na kuchangia
maendeleo ya wadau wa tiba asili.
Amesema changamoto kubwa iliyoletwa na Tafiti zinazofanywa na mradi
huo ni namna ambavyo sasa wanaweza wakachukua matokeo ya mradi huo ili kuyakuza kuleta maendeleo ya wadau binafsi katika kuongeza ubora na Masoko.

Prof. Mabiki amesema jambo lingine kubwa ambalo kama Chuo
wanajivunia na kufanikiwa kupata kifaa cha kisasa cha kupima kemikali za
mimea dawa, Madawa na vyakula ambacho kitaendeea kusaidia Watafiti,
Wanafunzi na wadau wengine kukikutumia katika kufanya tafiti
mbalimbali hapahapa nchini.

Mradi wa GRILI-DANIDA unatekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine(SUA)
kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS), Chuo Kikuu cha Sayansi na teknolojia Afrika cha Nelson
Mandela (NM-AIST), Chuo Kikuu cha Mzumbe, Shirika la Utafiti wa
Maendeleo ya Viwanda Tanzania(TIRDO), Taasisi ya taifa ya Utafiti wa
magonjwa ya Binadamu, NIMR, Chuo kikuu cha Copenhagen cha nchiniDenmark kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Denmark DANIDA.Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Walad Mwatawala akifungua mkutano huo, Pembeni yake ni Mkuu
wa Mradi wa GRILI Prof. Faith Mabiki.
Mtafiti Mkuu wa Mradi wa GRILI Prof. Faith Mabiki akiwasilisha malengo na mafanikio ya Mradi huo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Jeremy Kusiluka akitambulisha washiriki na ratiba ya siku hiyo ya kwanza ya mkutano huo.Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia mawasilisho ya tafiti mbalimbali zilizofanywa na mradi huo kupitia Wanafunzi wa Shahada ya Uzamivu na Uzamili.Picha ya pamoja ya Washirika wa Mradi Mkutano huo kutoka taasisi mbalimbali nchini na kutoka nje ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad