DKT. MOLLEL AMJIA JUU MENEJA WA BONDE LA MAJI KUWANYIMA MAJI WANANCHI WA SIHA. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 27, 2023

DKT. MOLLEL AMJIA JUU MENEJA WA BONDE LA MAJI KUWANYIMA MAJI WANANCHI WA SIHA.

 

Kutoka Siha Kilimanjaro.

Mbunge wa Jimbo la Siha na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amekasirishwa na kitendo cha kukosa maji wananchi wa jimbo la Siha kinachotakana na ugawaji usio sahihi wa maji unaofanywa na Meneja wa bonde katika chanzo cha maji.

Dkt. Mollel amesema Serikali ya Rais Samia kupitia Wizara ya maji imetimiza wajibu wake wa kuboresha miundombinu mipya ya maji, ila ugawaji wa maji kutoka kwenye chanzo unaofanywa ma meneja wa bonde hilo Bw. Segule Segule ndio unaopelekea uhaba wa maji ya matumizi kwa wananchi wa Siha ma maeneo ya karibu.

Amebainisha hayo alipofanya ziara ya kukagua hali ya chanzo cha maji katika bonde ma Pangani, alipoongozana na Mkuu wa Wilaya ya Siha pamoja na kamati yake ya Ulinzi na usalama.

Amesema, Sera ya maji inasema, kipaumbele cha kwanza cha ugawaji maji ni kwaajili ya matumizi kwa binadamu, namba mbili ni kwaajili ya mazingira na kipaumbele cha tatu ni kwaajili ya mambo mengine ikiwemo shughuli za uwekezaji.

Chakushangaza Meneja wa Bonde la pangani Bw. Segule Segule kipaumbele chake namba moja kaipa mambo mengine ambapo kampa 53%, huku wananchi wakipata 20% licha ya kuongezeka kwa kiasi kikubwa na namba tatu ni 0% yamepewa mazingira, amesema Dkt. Mollel.






 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad