WANAHARAKATI WANAWAKE NCHINI WAKATAA NENO WANAUME KWENYE MPANGO KAZI WA KUTOKOMEZA UKATILI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 26, 2023

WANAHARAKATI WANAWAKE NCHINI WAKATAA NENO WANAUME KWENYE MPANGO KAZI WA KUTOKOMEZA UKATILI

 

 


Na Humphrey shao, Michuzi Tv


Mtandao wa Wanawake katiba , Uchaguzi na Uongozi umeonesha kutokubaliana na pendekezo lankuingizwa Wanaume katika mpango kazi wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake, Watoto na Wanaume 2023-2027

Akizungumza na Waandishi wa Habari mmoja wa wajumbe wa tapo Hilo , Rebecca Gyumi Amesema kuwa wao kama tapo la utetezi wa Haki za Wanawake na wasichana nchini Tanzania .

"Tumesikitishwa sana na pendekezo lililotolewa la kujumuisha Wanaume kama kundi linalokabiliwa na Vitendo vya ukatili , sawa na Wanawake na watoto kwenye mpango kazi wa kitaifa wa kutokomeza ukatili na tungependa kuweka wazi kutokubaliana na pendekezo hili." Amesema Rebecca.

Rebecca Ametaja kuwa pendekezo hili limeanishwa kwenye Rasimu ya mpango kazi kama inavyosomeka "Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake Watoto na Wanaume 2023-2027."

Amesema kuwa Rasimu hii ya mpango kazi wa kitaifa yanaenda tofauti na lengo la kuwa na mpango kazi wa kitaifa uliojikita katika Kuleta mabadiliko ya kimfumo katika kwenye kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na watoto.

Rebecca Ametaja Msimamo wa tapo Hilo kuwa , Rasimu ya Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili ,utoe Neno wanaume na isomeke, mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili kwa Wanawake na watoto 2023 -2027.

Mpango kazi wa kitaifa wa kutokomeza ukatili , uendelee kuwatambua Wanawake na watoto kama kundi linaloathirika zaidi na ukatili wa kijinsia katika jamii na linalohitaji kuwekewa mifumo Wezeshi ilinkulinda dhidi ya Vitendo hivyo . Kwa kuwatambua wanaume kama focus ya mpango kazi mpango kazi wa kitaifa unakuwa umepoteza lengo lake.

Amesema wanaume waendelee kushiriki katika mapambano dhidi ya ukatili kwa Wanawake na watoto kama mabalozib, na sio kutambulika kama kundi linalokandamizwa.

Amesema Wanaume wanawaweza kuendelea kuripoti Vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya obkwa kutumia mifumo mingine ya Kisheria bila kuingilia jitihada ambazo zimekua zikifanyika kuwakomboa Wanawake na watoto ambao ndio waathirika wakubwa.

Utengenezwaji wa mpango kazi mpya uzingatie na kuongozwa na takwimu kuhusu Hali halisinya ukatili katika nchi yetu .jitihada zaidi ziwekwe kwenye kuboresha mifumo ya kuzuia na kushughulikia matukio ya ukatili kuimarisha uratibu na kuongeza rasilimali fedha kwenye afua zinazolenga kutokomeza ukatili kwa Wanawake na watoto.

Kwa upande wake mratibu wa kitaifa wa tapo Hilo la Wanawake Dr.Evemaria Semekafu Amesema wao kama Wanaharakati wa Masuala ya Wanawake na watoto wameshangaa kuona Neno Wanaume katika kichwa hicho Cha habari wakati mchakato mzima aukuwahusisha Wanaume.

Dunia nzima inaona Tanzania kama mfano wa kupigania Haki za Wanawake na watoto Leo waone kuwa tunawaweka katika mizani Moja na Wanaume hili litaweza kutunyima fursa katika Mambo ya kimataifa.
Rebeca Gyumi akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Tamko la Wanaharakati Wanawake.Dr.Evemaria Semakafu akifafanua mchakato mzima ulivyokuwaMkurugenzi wa Tamwa Dr.Rose Reuben akieleza namna takwimu zilivyo juu kwa ukatili wa Wanawake na watoto nchiniViongozi wa Wanaharakati Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja wakitoa Tamko lao 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad