RUVUMA WAADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA RAIS SAMIA KWA KUPANDA MITI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 28, 2023

RUVUMA WAADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA RAIS SAMIA KWA KUPANDA MITI

 

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaongoza wananchi kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupanda miti katika shule za Msingi na sekondari Mashujaa Manispaa ya Songea.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha zoezi hilo,Kanali Laban amesema Mkoa umeamua kuifanya shughuli ya kupata miti ya matunda ikiwa ni maalum kuunga mkono siku ya kuzaliwa kwa Rais.

“Nichukue fursa hii kumtakia heri na afya tele Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa,kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma tunampongeza sana,Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda ili aendelea kuliongoza Taifa letu la Tanzania’’,alisema

Amesema mara nyingi Rais Dkt.Samia amekuwa wanahimiza watanzania kupanda miti ya matunda hivyo katika tukio hilo ,Kanali Thomas ameongoza kupanda miti ya matunda aina ya miparachichi na mipera katika shule za msingi Mashujaa na shule ya sekondari Mashujaa. “Jambo muhimu sio tu kupanda miti,bali kuhifadhi na kuilinda ili miti hiyo iweze kukua,miti hii kwa kuwa ni ya matunda inaweza kutumika kama chakula kwa wanafunzi hivyo kujenga afya za wanafunzi na wal’mu’’,alisema RC Thomas.

Mkuu wa Mkoa amewahimiza wananchi wote mkoani Ruvuma kuendelea kupanda miti nyumbani na kwenye mashamba ambapo amesema mashamba mengi ya kahawa hivi sasa yamebakia vipara baada ya miti kukatwa hivyo amewashauri wakulima kuhakikisha mashamba yao
yanapandwa miti.

Amesema uzinduzi wa Kampeni ya wiki ya upandaji miti kimkoa ilifanyika Januari Mosi mwaka huu ambapo jumla ya miti milioni 1.1 ilipandwa ambapo amesema zoezi la upandaji miti ni endelevu hadi mvua zitakapoishia.

Afisa Maliasili Mkoa wa Ruvuma Africanus amesema kwenye zoezi hilo maalum lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa jumla ya miti 400 imepandwa kati ya hiyo miti ya matunda 200 na miti ya kupanda kwenye mipaka 200.

Mkoa wa Ruvuma kwa mwaka 2023 unatarajia kupanda miti ya aina mbalimbali zaidi ya milioni nane ambayo inapandwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Taasisi za Serikali, Taasisi binafsi na
wananchi. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akiwa wajumbe wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Ruvuma na wilaya ya Songea wakijiandaa kushiriki zoezi la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kuzal,iwa Rais Dkt.Samia Suluhu HassanMkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Mashujaa Manispaa ya Songea muda mfupi kabla ya kuanza kazi ya kupanda miti kwenye viwanja vya shule za msingi  Mashujaa na sekondari ya Mashujaa

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akipanda miti  wa mpalachichi katika shule ya msingi Mashujaa Manispaa ya Songea ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Rais Dkt Samia Suluhu Hasaan,katika tukio hilo maalum jumla ya miti 400 imepandwa

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki akipanda miti wa matunnda katika shule ya sekondari Mashujaa Manispaa ya Songea Afiisa Uhamiaji wa Mkoa wa Ruvuma Tunu


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad