Ni kufuatia Maamuzi ya kikosi kazi Cha Mawaziri 8 kilichoshughulikia Mgogoro uliokuwepo baina ya Wilaya za Kisarawe na Ilala.
- Asema Serikali Sikivu ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefuata maoni na matakwa ya Wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla Leo January 13 ameitangaza Kata ya Zingiziwa na Wananchi wake kuwa Sehemu ya Wilaya ya Ilala kufuatia kikosi kazi Cha Mawaziri 8 kumaliza mgogoro wa mipaka wa muda mrefu uliokuwepo.
RC Makalla amesema maamuzi hayo yamezingatia vigezo mbalimbali ikiwemo ukaribu na uwepo wa huduma nyingi za kijamii Wilaya ya Ilala kuliko Wilaya ya Kisarawe.
Akitangaza Maamuzi hayo wakati wa Mkutano wa hadhara wa Wananchi wa Kata hiyo, RC Makalla amesema Serikali sikivu ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeangalia na kuzingatia matakwa ya Wananchi wake.
Kuhusu suala la Mgogoro wa mipaka kwenye Msitu wa Kazimzumbwi, RC Makalla amesema mipaka ya Msitu huo itatafsiriwa Ardhini (Majira ya Nukta) ambapo timu Ya Wataalamu itapita na kuweka mawe na mwisho wa siku maamuzi yatatangazwa.
Aidha RC Makalla amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya Kisarawe kuweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kesi na Watuhumiwa waliokuwa wameshikiliwa kwenye vituo vya Polisi Kisarawe kesi zinamalizwa kwa mujibu wa Sheria.

No comments:
Post a Comment