PRECIOUS MASSAWE ATWAA U MISS MAZUBU 2023 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 5, 2023

PRECIOUS MASSAWE ATWAA U MISS MAZUBU 2023

 

 

Na Mwandishi wetu, Mirerani

MWANAFUNZI wa darasa la pili wa shule ya awali na msingi Glisten ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Precious Mark Massawe ameshinda taji la Miss Mazubu 2023.

Precious Massawe ameshinda ubingwa huo baada ya kuwabwaga mabinti wenzake katika michuano hiyo iliyoshirikisha wasichana nane wanyange wa mji mdogo wa Mirerani.

Mshindi huyo alitangazwa kushinda nafasi hiyo na jaji mkuu wa mashindano hayo Jema Lilama (Kichuna wa Kimakonde) baada ya kuonyesha vazi la ubunifu na vazi la kutokea.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani, Adam Kobelo alimkabidhi Miss Mazubu 2023 Precious Massawe, zawadi ya kitita cha shilingi taslimu 250,000.

Pia, Kobelo alimpatia mshindi huyo zawadi ya fulana yenye nembo ya Mazubu Grand Hotel na daftari kubwa la kuandikia somo moja atakaloamua kuandikia.

Kwa upande wa Mr Mazubu 2023, Kobelo alimpatia mshindi wa taji hilo Andrew Lyimo kiasi cha fedha taslimu shilingi 250,000.
Pia, Andrew Lyimo alipatiwa zawadi ya fulana yenye nembo ya Mazubu Grand Hotel na daftari kubwa la kuandikia somo moja atakaloamua kuandikia. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad