Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Askari wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa Polisi Janeth Magomi wameshiriki kupanda miti Elfu moja ikiwa ni hatua ya kukabiliana na mabadiliko tabia Nchi.
Askari wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa Polisi Janeth Magomi wameshiriki kupanda miti Elfu moja ikiwa ni hatua ya kukabiliana na mabadiliko tabia Nchi.
Shughuli hiyo imefanyika leo Ijumaa Januari 13,2023 ambapo askari wa Polisi kwa kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wadau mbalimbali wamepanda miti Mia mbili (200) katika eneo la kambi ya kutuliza Gasia (FFU) jina maarufu Bwalo la Polisi pamoja na miti Mia nane kwenye eneo la Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga .
Akizungumza baada ya kupanda miti hiyo katika eneo la Bwalo la Jeshi la Polisi na kwenye mazingira yanayozunguka Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga eneo la Mwawaza,kamanda Magomi amesema hatua hiyo ni mkakati unaolenga kuhifadhi mazingira.
Kamanda Magomi Magomi amefafanua zaidi kuwa pamoja na majukumu mengine lakini utunzaji wa mazingira ni mpango endelevu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga.
Ameeleza kuwa hatua hiyo pia ni kuunga mkono serikali kupitia kampeni ya upandaji miti ambapo amesema jeshi hilo limejipanga kukabiliana na mazingira ikiwemo kuwachukulia hatua watu wanaobainika kuharibu mazingira.
“Tupo hapa kwa ajili ya kumuunga mkono mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika suala zima la kupambana na mabadiliko ya tabia Nchi, Shinyanga ya kijani inaweekana Shinyanga bila ukame inawezekana”.
“Tupo hapa kwa ajili ya kumuunga mkono mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika suala zima la kupambana na mabadiliko ya tabia Nchi, Shinyanga ya kijani inaweekana Shinyanga bila ukame inawezekana”.
“Jeshi la Polisi tumejipanga kupambana na mazingira lakini tunaendelea kuwaunga mkono viongozi wetu kuhakikisha kwamba tutaendelea kupanda miti na zoezi hili ni endelevu na wale wote ambao wataenda kinyume kukata miti bila kibali tuko tayari kuwashughulikia”.amesema kamanda Magomi
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ambaye ameshiriki katika zoezi la kupanda miti hiyo, ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuhusu wajibu wa kuzuia uharibifu wa mazingira, ikiwa ni pamoja na kuepuka ukataji holela wa miti huku akiwasisitiza wakazi wa Manispaa ya Shinyanga kuzuia uzurulaji wa mifugo na kwamba jukumu la utunzaji mazingira nila kila mtu.
“Tuhakikishe miti hii inakuwa na kuhakikisha kwamba kampeni hii ya miti inaendelea katika Wilaya ya Shinyanga niendelee kuwaomba wananchi katika maeneo ya kata zetu zote ni marufuku kukata miti bila kibali na wale wote ambao wanatembeza mifugo kwenye maeneo mbalimbali ya mitaa na vijiji katika Halmashauri yetu ya Manispaa ya Shinyanga ni marufuku kupitisha mifugo kwa sababu kwanza inachafua mazingira lakini pili inakula miti yetu tunataka kuona miti yetu inaendelea kukua”.
“Sheria zipo za Halmashauri kuhakikisha kwamba wale wote ambao wanatembeza mifugo nah ii miti inaharibika wanachukuliwa hatua pamoja na wale wa mbuzi kwahiyo wananchi wote wahakikishe kwamba wanafuga mifugo kwenye nyumba zao”.amesema DC Mboneko.
Afisa mazingira wa Halmashauri ya manispaa ya shinyanga Ezra Manjerenga amesisitiza umuhimu wa upandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko alama itakayodumu kizazi hadi kizazi.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John ameshukuru na kupongeza hatua hiyo ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ambapo ameahidi kuilinda ili kuja kuleta manufaa katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Baadhi ya wadau walioshiriki katika shughuli hiyo ya upandaji wa miti wakiwemo viongozi wa serikali za mitaa pamoja na Jeshi la jadi Sungusungu wameahidi kushiriki katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira.
No comments:
Post a Comment