WAKAZI WA MIKOA YA PWANI NA DAR ES SALAAM MILIONI 11 WANAHITAJI MAJI KILA SIKU -HALIMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 22, 2023

WAKAZI WA MIKOA YA PWANI NA DAR ES SALAAM MILIONI 11 WANAHITAJI MAJI KILA SIKU -HALIMA

 

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV 

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu imesema kuwa Wakazi wa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam Milioni 11 wanahitaji maji kila siku hivyo kila mmoja ana nafasi ya kulinda vyanzo vya maji juu ya ardhi na chini Ardhi ili kuwa na uhakika wa kupata maji hayo.

Hayo aliyasema Afisa wa Kidakio cha Pwani wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu (WRBWB) Halima Faraj wakati wa kikao cha Jukwaa la Kidakio cha Pwani walikutana kwa ajili ya kuangalia na namna ya kuhifadhi maji na kulinda vyanzo vya maji kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Halima amesema Jukwaa ni muhimu katika utekelezaji wa mikakati ya usimamizi wa maji kwenye vyanzo kutokana na wadau wake wanatoka kwa kwenye jamii na kwenda kuwa mabalozi.

Amesema Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu imeanzisha majukwaa ili kushirikiana katika usimamizi wa vyanzo vya maji katika kufanya huduma za upatikanaji wa maji zinakuwa endelevu.

Aidha amesema Serikali ya awamu ya Sita  chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imekuwa ikisisitiza utunzaji wa mazingira ya vyanzo vya maji ya kutaka wananchi kuacha kuharibu vyanzo vya maji vilivyopo.

Amesema kuwa Mabadiliko ya Tabianchi ni kutokana na uhalibifu wa mazingira ambapo uhalibifu huo ndio kisasi ya kuwepo mabadiliko hayo ya tabianchi.

Amesema kuwa wananchi wakichimba visima bila kupata vibali ambao ni kosa la kisheria kutokana na maji ya chini ardhi kuna vitu vya kitaalamu vinatakiwa kufanyika.

Halima amesema mifugo na na shughuli za kilino kwenye kando kando ya mito ndio changamoto kwenye vyanzo vya maji ndio wakati mwengine kidakio cha cha Pwani kinakosa maji.
Afisa wa Kidakio cha Pwani wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu (WRBWB) Halima Faraj akizungumza katika Kikao  cha Jukwaa la Kidakio cha Pwani kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Kidakio cha Pwani wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu (WRBWB) Halima Faraj akitoa mada kwenye kikao  cha Jukwaa la Kidakio cha Pwani kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji Will Mwaluvanda akitoa mada kwenye kikao cha Jukwaa la Kidakio cha Pwani kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Afisa Maendeleo Mwandamizi wa Kidakio cha Pwani wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Hhau Sarwatt akitoa majumuisho ya Kikundi cha Mazingira kilichojadili njia bora ya uhifadhi wa maji kwenye vyanzo vya maji kwenye kikao cha  Jukwaa la Kidakio  cha Pwani jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Kidakio cha Pwani Anna Kimaro akizungumza mikakati ya Jukwaa hilo kwenye kikao kilichifanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya kamati ya utekelezaji ya Jukwaa la Kidakio Pwani.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Jukwaa la Kidakio cha Pwani na  Kamati ya Utelekezaji mara baaada ya kufungwa kwa kikao. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad