SIMBA SC YASHUSHA MBUKINABE, NI KIUNGO MKABAJI… - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 15, 2023

SIMBA SC YASHUSHA MBUKINABE, NI KIUNGO MKABAJI…

Na Bakari Madjeshi, Michezo 

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wameendelea na maboresho ya Kikosi chao baada ya kutangaza kumsajili Kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso, Hamed Ismael Sawadogo kwa mkataba wa miaka miwili, Sawadogo alikuwa anacheza Klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco.

Sawadogo anayecheza nafasi ya Kiungo cha Ukabaji (Defensive Midfielder) tayari amekamilisha usajili Simba SC na atajiunga na wenzake siku ya Jumanne baada ya kurejea nyumbani Tanzania wakitokea kambi katika ardhi ya Falme za Kiarabu, Dubai.Sawadogo mara nyingi anatumia mguu wa kushoto amewahi pia kucheza timu mbalimbali barani Afrika, ENPPI ya nchini Misri, US Ouagadougou ya nyumbani kwao Burkina Faso.

Simba SC imekamilisha usajili wa Kiungo huyo akiwa wa pili baada ya kukamilisha usajili wa Mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi, Saido Ntibazonkiza ambao wote watatumika katika mashindano mbalimbali ambayo timu hiyo inashiriki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad