DC MOYO MARUFUKU KAMPUNI ZA ULINZI KUAJIRI WASIOPITIA MAFUNZO YA KIJESHI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 4, 2023

DC MOYO MARUFUKU KAMPUNI ZA ULINZI KUAJIRI WASIOPITIA MAFUNZO YA KIJESHI

 

 


Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wahitimu wa mafunzo ya mgambo juu ya serikali ya wilaya ya Iringa kuwapambania kupata ajira kwenye kampuni za Ulinzi zizopo katika wilaya hiyo
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akikagua gwaride la askari mgambo ambao wamemaliza mafunzo ya awali ya kijeshi tayari kwa ajili ya kufanya kazi za Ulinzi kwenye makampuni mbalimbali ya ulinzi

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akikagua gwaride la askari mgambo ambao wamemaliza mafunzo ya awali ya kijeshi tayari kwa ajili ya kufanya kazi za Ulinzi kwenye makampuni mbalimbali ya ulinziNa Fredy Mgunda, Iringa.


SERIKALI ya wilaya ya Iringa imezitaka kampuni za Ulinzi kuajiri wafanyakazi waliopitia mafunzo ya kijeshi ili kuboresha ufanisi wa kazi katika sekta ya ulinzi wa mali za UMMA, serikali,watu binafsi na mashirika binafsi.

 

Akifunga mafunzo ya Jeshi la akiba katika kata ya Masaka mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa kitendo cha makampuni ya ulinzi yaliyopo wilaya ya Iringa kuajiri walinzi wasio na mafunzo kinakinzana na taratibu na sheria zilizopo, huku kikiwanyima fursa askari waliopitia mafunzo ya kijeshi.

 

Moyo aliliagiza Jeshi la Polisi kuanzisha ukaguzi maalum dhidi Makampuni ya ulinzi Wilayani Iringa ili kujiridhisha endapo walioajiriwa Kwa kazi ya Ulinzi wamekidhi vigezo vinavyotambuliwa kwa mujibu wa sheria.


Alizitaka kampuni za Ulinzi zizopo wilaya ya Iringa kuwaondosha kazini wafanyakazi wasiopitia mafunzo ya Jeshi,Kabla ya Serikali kuchukua hatua ya kuyafutia leseni makampuni hayo.


Kiongozi huyo ameeleza mpango wa Serikali ya wilaya katika kusaidia kundi kubwa la vijana waliohitimu mafunzo hayo..

 

Moyo alimazia kwa kusema kuwa Serikali haiwezi kuvumilia kuona makampuni hayo yakikiuka sheria kwa makusudi akibainisha kuwa kitendo cha kuajiri watu wasiopitia mafunzo kuwa ni chanzo cha uhalifu katika maeneo mbalimbali


Kwa upande wao wahitibu wa mafunzo haya ya jeshi la akiba katika risala yao wameeleza miongoni mwa changamoto kuu ni kukosa ajira katika makampuni ya ulinzi kwani makampuni yaliyo mengi yanaajiri watu wasiopitia mafunzo ya jeshi

 

Naye Diwani wa kata ya masaka Methew Nganyagwa akimualika Mgeni wa heshima katika hafla hiyo amesema mafunzo hayo yamekuwa na tuija kubwa ya kimaendeleo katika kata hiyo

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad