MKOA WA RUVUMA KULIMA HEKTA ZAIDI YA 900 ZA MAZAO MBALIMBALI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 26, 2023

MKOA WA RUVUMA KULIMA HEKTA ZAIDI YA 900 ZA MAZAO MBALIMBALI

 

MKOA wa Ruvuma umelenga kulima jumla ya hekta 930,082 za mazao ya chakula,biashara na mazao ya bustani katika msimu wa kilimo wa mwaka 2022/2023.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema hekta hizo zinatarajia kutoa mavuno ya tani 1,965,072 na kwamba kati ya hekta hizo,kilimo cha mazao ya chakula ni hekta 569,070 zinazotarajia kutoa mavuno ya tani 1,638,808.

Amesema katika mazao ya biashara zinatarajiwa kulimwa hekta 337,572 ambazo zinazotarajiwa kutoa mavuno tani 102,379 na kwa mazao ya bustani zinatarajiwa kulimwa hekta 23,399 zinazotarajiwa kutoa mavuno tani 223,886.

Hata hivyo amesema hali ya upatikanaji wa chakula mkoani Ruvuma ni nzuri kwa kuwa ipo katika kiwango cha utoshelevu na ziada kwa miaka 12 mfululizo.

“Chakula kilichozalishwa katika msimu wa 2021/2022 kinatumika kwa msimu huu wa 2022/2023 ambapo mazao ya chakula yalizalishwa tani 1,256,362 na mahitaji ya chakula ndani ya Mkoa kwa msimu wa 2022/2023 ni tani 469,172 na kuufanya Mkoa kuwa na ziada ya chakula tani
787,190’’,alisema Kanali Thomas.

Akizungumzia upatikanaji wa mbolea ya ruzuku mkoani Ruvuma,Kanali Thomas amesema katika msimu wa mwaka 2022/2023 Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania(TFRA) unatekeleza mpango wa utoaji mbolea ya
ruzuku.

Amesema hadi kufikia Januari 13,2023,Mkoa wa Ruvuma kupitia vitabu umesajili jumla ya wakulima 278,010 kati ya lengo la kusajili wakulima 428,288 na kwamba jumla ya wakulima 272,624 wameshaingizwa kwenye mfumo sawa na asilimia 98 na walianza kupata mbolea tangu Agosti 2022
zoezi la usajili lilipoanza.

Hata hivyo amesema katika msimu wa mwaka 2022/2023 Mkoa wa Ruvuma umelenga kusambaza mbolea ya ruzuku zaidi ya tani 50,000 ambapo hadi sasa Mkoa umesambaza zaidi ya tani 42,000 kupitia
Kampuni na mawakala wa mbolea.

Mkoa wa Ruvuma kwa miaka minne mfululizo umeendelea kuwa kapu la chakula la Taifa baada ya kuongoza kitaifa katika uzalishaji wa chakula nchini.
shamba la mahindi katika kijiji cha Lipokela wilayani Songea ambalo limelimwa msimu huuMkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akiwa ofisini kwake mjini Songea 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad